Feb 17, 2020 02:42 UTC
  • Nancy Pelosi: Kila mgombea wa chama cha Democrat ni bora kuliko Trump

Nancy Pelosi, Spika wa Bunge la Wawakilishi la Marekani amesema kuwa mgombea yeyote wa chama cha Democrat katika uchaguzi wa 2020 kuelekea White House, ni bora kumliko Rais Donald Trump.

Pelosi ameyasema hayo katika mahojiano na kanali ya CNN ambapo amemtaja Donald Trump kuwa mvamizi wa White House na kwamba bila shaka rais huyo atashindwa katika uchaguzi ujao wa rais. Kadhalika Spika huyo wa Bunge la Wawakilishi la Marekani amesisitiza kuwa: "Tukifumbia macho ni nani atakuwa mshindi wa uchaguzi ndani ya chama cha Democrat, ninasema bila kusita kuwa Trump atashindwa tu katika uchaguzi wa 2020. Mteuliwa wa mwisho wa uchaguzi wa ndani ya chama cha Democrat katika majimbo tofauti, ndiye atakayechuana na Rais Donald Trump katika uchaguzi wa tarehe tatu Novemba 2020.

Nancy Pelosi, Spika wa Bunge la Wawakilishi la Marekani

Kabla ya hapo pia Nancy Pelosi, Spika wa Bunge la Wawakilishi la Marekani alinukuliwa akisisitiza kuwa, mwaka ujao wa 2021 Trump hatokuwa tena rais wa Marekani. Pelosy aliyasema hayo alipozungumza na televisheni ya ABC NEWS, mwanzoni mwa mwezi jana.

Maoni