Feb 17, 2020 02:43 UTC
  • Malalamiko na ukosoaji kwa ongezeko la mashambulizi ya anga ya Marekani dhidi ya raia Afghanistan

Ongezeko la hasara linalotokana na mashambulizi ya anga ya askari wa Marekani dhidi ya raia wa Afghanistan, limekabiliwa na malalamiko na ukosoaji mkubwa wa shakhsia, wananchi na wabunge wa nchi hiyo.

Katika uwanja huo Hamid Karzai, rais wa zamani wa Afghanistan ametoa taarifa ambayo imekosoa vikali mashambulizi ya anga yaliyofanywa Ijumaa iliyopitwa na askari hao vamizi wa Kimarekani kwa kuwalenga raia wa kawaida mashariki mwa Kabul, mji mkuu wa nchi hiyo. Katika taarifa hiyo Karzai amesema kuwa, badala ya Marekani kuwaua raia wasio na hatia wa Afghanistan, ni bora ijikite kwenye mwenendo wa amani na kuhitimisha vita nchini humo. Kabla ya hapo pia rais huyo wa zamani wa Afghanistan alinukuliwa akisema kuwa, mashambulizi ya Marekani dhidi ya maeneo ya serikali na raia wa kawaida ni sababu kuu ya kuongezeka chuki na hasira ya wananchi dhidi ya askari hao wa kigeni. Itakumbukwa kuwa katika mashambulizi ya anga ya Ijumaa iliyopita yaliyofanywa na askari wa Marekani dhidi ya magari mawili eneo la Sorkh Roud, jimbo la Nangarhar mashariki mwa Afghanistan, kwa akali raia 10 waliuawa.

Askari vamizi wa Marekani nchini Afghanistan

Naye Atwaullah Khogiyani, Msemaji wa Gavana wa jimbo la Nangarhar sambamba na kuthibitisha habari ya hujuma hiyo ya kinyama ya askari vamizi wa Kimarekani katika eneo la Sorkh Roud alisema kuwa, wahanga wote wa shambulizi hilo walikuwa raia wa kawaida. Aidha katika mashambulizi ya ndege za kivita na zile zisizo na rubani za Marekani katika maeneo tofauti ya nchi hiyo ikiwemo Farah, Herat, Kunduz na Badghis yaliyotekelezwa mwaka jana pekee jumla ya raia wa kawaida 750 waliuawa au kujeruhiwa. Kuongezeka mashambulizi ya askari hao vamizi wa Marekani katika maeneo ya makazi nchini Afghanistan, kumeibua hasira kali ya wabunge, shakhsia wa kisiasa, kidini na raia wa kawaida wa nchi hiyo.

Tags

Maoni