Feb 20, 2020 04:34 UTC
  • Trump apatwa na hasira kali baada ya maseneta wa Democrat kukutana na Javad Zarif

Rais Donald Trump wa Marekani amekasirishwa mno na kitendo cha maseneta wa chama cha Democrat kukutana na Mohammad Javad Zarif, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran na kudai kuwa mikutano ya wanasiasa wa chama hicho na Zarif, ndio sababu inayoifanya Tehran isikubali mazungumzo na Washington.

Trump ambaye anakosolewa vikali kutokana na siasa zake mbovu kuihusu Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameandika kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter kwamba kitendo cha baadhi ya wanasiasa wa Democrat kukutana na Zarif, ndio sababu inayoifanya Tehran kukataa kufikia mapatano mapya na Marekani. Akizungumzia vikao vya 'Chris Murphy' Seneta wa Democrat na 'John Kerry', Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje wa Marekani pamoja na Mohammad Javad Zarif, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameandika kwenye ukurasa wake wa kijamii wa Twitter kwamba: "Kerry na Murphy wamekiuka sheria ya Logan." Sheria ya Logan inazuia mazungumzo yasiyoruhusiwa ya shakhsia wasio wa kiserikali wa Marekani na serikali nyingine za kigeni.

Chris Murphy' Seneta wa Democrat

Idadi kadhaa ya wanachama wa Democrat wakiongozwa na Chris Murphy' Seneta wa jimbo la Connecticut walikutana na Mohammad Javad Zarif, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran kando ya mkutano wa Usalama wa mjini Munich, Ujerumani. Kufuatia suala hilo Abbas Mousavi, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran alisema kuwa kikao hicho kinahesabiwa kuwa sehemu ya udiplomasia wa kijamii. Aliongeza kuwa daima Zarif amekuwa akisisitiza kuwa baadhi ya wawakilishi wa bunge la Kongresi ya Marekani wanaoomba vikao na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, huwa anawakubalia na kukutana nao ambapo huwa anawabainishia uhalisia wa mambo kuhusu misimamo ya Iran na hali ya mambo ya Asia Magharibi.

Tags

Maoni