Feb 26, 2020 04:45 UTC
  • Pakistan: Tuko huru kutumia silaha ya aina yoyote ya kivita

Naibu Kamanda Mkuu wa Jeshi la Anga la Jeshi la Pakistan amesema kuwa, jeshi la nchi hiyo liko huru kutumia silaha yoyote ya kivita na haihitaji kuomba ruhusa kwa nchi yoyote ile.

Amir Shah aliyasema hayo Jumanne ya jana ambapo akiashiria kwamba Pakistan ipo huru kutumia silaha yoyote ya kivita, amesema kuwa, katika uwanja wa kulinda ardhi ya nchi hiyo, Islamabad haihitaji kuomba idhini kwa nchi yoyote kuhusu silaha inayofaa kuitumia. Naibu Kamanda Mkuu wa Jeshi la Anga la Jeshi la Pakistan ameyasema hayo sambamba na kumbukumbu za kwanza za vita vya anga vilivyojiri kati ya nchi hiyo na India ambapo akiashiria ndege za kivita zilizonunuliwa kutoka Marekani amesema kuwa, ikihitajika Pakistan itatumia zana zake zote zikiwemo ndege hizo tena bila ya idhini ya nchi yoyote ile. 

Mzozo kati ya India na Pakistan

Akiendelea Amir Shah ametupilia mbali madai yaliyotolewa na serikali ya India ya kutunguliwa na nchi hiyo ndege ya kivita aina ya F 16 ya Pakistan na kusema kuwa ndege zake zote za kivita aina ya F 16 zipo salama. Baada ya shambulio la anga lililotekelezwa na jeshi la India katika ardhi ya Pakistan mwanzoni mwa mwaka jana na jibu la kijeshi lililotolewa na Islamabad, kuliibuka mzozo katika uhusiano wa kisiasa kati ya nchi mbili sambamba na kuzuka mapigano ya mpakani baina yao.

Tags

Maoni