Feb 26, 2020 12:53 UTC
  • Chanjo ya kula iliyotengezwa China yatoa tumaini la kudhibitiwa kikamilifu kirusi cha corona

Wizara ya Afya ya China imetangaza kuwa, chanjo ya kula iliyotengezwa nchini humo imeongeza matumaini ya kudhibitiwa kikamilifu kirusi kipya cha corona cha COVID-19.

Taarifa iliyotolewa leo na Wizara ya Afya ya China imeeleza kuwa, baada ya kutibiwa na kupona watu wengine elfu tatu katika muda wa saa 24 zilizopita na kutengezwa chanjo ya kula, matumaini ya kukidhibiti kikamilifu kirusi cha corona nchini humo yamezidi kuongezeka.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, hadi sasa watu elfu 30 miongoni mwa waliokuwa wameambukizwa kirusi hicho nchini humo wametibiwa na kupona.

Maambukizi ya kirusi cha corona yalianzia katika mji wa Wuhan nchini China Desemba mwaka uliopita wa 2019 na inavyoonesha chanzo chake ni wanyama wasio wa kufuga.

Mbali na mikoa 30 ya China, hivi sasa kirusi hicho kimesambaa kwenye nchi zaidi ya 36 duniani zikiwemo za eneo la Asia Magharibi.

Watu wasiopungua 2,665 wamefariki dunia hadi sasa nchini China kutokana na ugonjwa unaosababishwa na kirusi hicho.

Wakati huohuo Wizara ya Afya, Tiba na Mfunzo ya Utabibu ya Iran imetangaza kuwa idadi ya watu walioambukizwa kirusi cha corona hapa nchini imefikia 139.

Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Habari ya Wizara ya Afya Kianush Jahanpur amesema: Idadi ya waliofariki kwa ugonjwa unaosababishwa na kirusi hicho imefikia watu 19.../

 

Tags

Maoni