Mar 26, 2020 03:50 UTC
  • Madai ya Pompeo: China na Russia zinaficha taarifa za virusi vya Corona

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani amedai kuwa serikali za Russia na China zinajiepusha kutoa taarifa sahihi za virusi vya Corona.

Mike Pompeo ameyasema hayo katika mahojiano ya kipindi cha redio cha 'Washington Watch' ambapo akikariri madai yake ya huko nyuma juu ya kucheleweshwa na China taarifa za maradhi hayo, amesema kuwa hali hiyo inahatarisha maisha ya maelfu ya watu.

Kadhalika Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani ameendelea kudai kuwa Iran na Russia pia zinatoa taarifa zisizo sahihi kuhusu virusi vya Corona.

Ugonjwa wa Corona ambao umeivamia kwa namna ya kutisha Marekani

Madai hayo ya Pompeo ni radiamali kuhusu tuhuma zilizoelekezwa kwa Washington kwamba jeshi la Marekani ndio lililozalisha na kusambaza virusi vya Corona ambavyo vimeikumba pia chi hiyo.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani amesema kuwa serikali ya Washington iko chini ya mashinikizo makali ya ndani yanayosababishwa na usimamizi mbaya wa idara za kukabiliana na Corona.

Aidha ametoa vitisho kwamba baadaye Marekani itachukua uamuzi muhimu kuhusu uhusiano wa China na Marekani utakavyokuwa.

Tags

Maoni