Mar 30, 2020 02:26 UTC
  • Corona yawaelemea Wazayuni, waomba msaada kwa Ujerumani, wakataliwa

Baada ya wimbi la maambukizi ya corona kuukumba utawala wa Kizayuni wa Israel, viongozi wa utawala huo ghasibu wamekuwa wakihaha kutafuta msaada kila sehemu ikiwemo Ujerumani ambako Kansela wa nchi hiyo Angela Merkel amekataa kuisaidia Israel akisisitiza kuwa Ujerumani yenyewe ina upungufu wa vifaa.

Shirika la habari la IRNA limetangaza kuwa, Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel amepigiwa simu na Waziri Mkuu wa Israel, Benjamn Netanyahu akiiomba Berlin iusaidie utawala wa kizayuni vifaa vya kupambana na corona kama vile vya kuwasaidia wagonjwa kupumua, lakini Angela Merkel amekataa kutuma msaada wowote kwa Israel akisema kuwa Ujerumani yenyewe ina upungufu wa vifaa hivyo.

Kansela wa Ujerumani amesema, nchi yake imeiazima Ufaransa mamia ya vifaa vya kukabiliana na corona, hivyo haiwezi kutoa msaada mwingine kwani yenyewe hivi sasa ina vifaa pungufu.

Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu

 

Kwa mujibu wa takwimu rasmi, Ukitoa Marekani, Italia, China, na Uhispania; Ujerumani ni nchi ya tano kwa kuwa na maambukizi mengi zaidi ya kirusi cha corona duniani. 

Kwa mujibu wa takwimu rasmi, zaidi ya askari elfu sita wa utawala wa Kizayuni wa Israel wamewekwa chini ya karantini hadi hivi sasa.

Jumanne usiku pia, Benjamin Tetanyahu, Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni alisema kuwa mwezi mmoja ujao karibu watu milioni moja kati ya watu wote milioni nane na 600 wanaoishi katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na Wazayuni, wataambukizwa kirusi cha corona na karibu watu elfu 10 watapoteza maisha kutokana na ugonjwa huo hatari wa COVID-19.

Tags

Maoni