Apr 05, 2020 02:52 UTC
  • Jenerali Mmarekani amlalamikia mkwe wa Trump kufanya ubaguzi katika vifaa vya corona nchini Marekani

Kamanda mmoja Mmarekani amelalamikia vikali siasa za kibaguzi za mkwe wa rais wa nchi hiyo, Donald Trump za kuwabagua Wamarekani katika kugawa vifaa vilivyobakia vya kinga ya corona nchini Marekani.

Gazeti la Daily Mail limemnukuu Luteni Jenerali Russel Honoré kamanda wa jeshi la Marekani akisema hayo na kumlaumu vikali mkwe wa Donald Trump, Jared Kushner kwa jinsi anavyofanya ubaguzi katika kugawa vifaa vya kujikingina na corona. 

Jenerali Honoré ambaye baada ya kimbunga cha Katrina alitoa mchango mkubwa wa kuljenga upya jimbo la New Orleans ameongeza kuwa, Kushner hajui anachokisema na hata timu yake iliyoteuliwa na Trump kusimamia vifaa vya matibabu wakati huu wa corona huko Marekani, imechanganyikiwa na haijui itoe kipaumbele kwa nani.

Siku ya Alkhamisi, Kushner aliteuliwa na baba mkwe wake, Donald Trump kusimamia vifaa hivyo vya kupambana na ugonjwa wa COVID-19 na wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu akiba ya vifaa hivyo, Kushner alisema: Hii ni akiba yetu sisi na haikupangwa kuwa akiba ya majimbo ya Marekani kama ambavyo pia si kwa ajili ya matumizi ya majimbo hayo.

Donald Trump na mkwewe, Jared Kushner

 

Matamshi hayo ya Kushner yamekosolewa vikali na wakuu wa majimbo na vyombo vya habari vya Marekani suala ambalo lilimlazimisha Trump atenge wakati maalumu wa kumtetea mkwe wake aa kupindisha maneno akisema, sisi si maafisa wa usafirishaji.

Televisheni ya MSNBC imeripoti kuwa Kushner amevipeleka vifaa hivyo kwa mashirika binafsi na si kwa hospitali ambazo zinahitajia mno vifaa hivyo hivi sasa. 

Marekani sasa hivi inaongoza kwa mbali maambukizi ya corona duniani huku wakuu wa serikali ya Trump wakionesha wazi kuchanganyikiwa wakisema hawajui kitatokea nini kama maghala ya vifaa vya kiistratijia katika majimbo 50 ya Marekani vitakwangurwa na kisibakie hata kifaa kimoja. 

Maoni