Apr 06, 2020 02:34 UTC
  • Marekani na Ulaya zakumbwa na changamoto katika kukabiliana na Corona

Mjumbe wa Baraza Kuu la Waislamu nchini Ujerumani ameelezea hali mbaya ya nchi za Ulaya katika kukabilina na virusi vya Corona na kubainika wahka unaotokana na maradhi hayo katika jamii ya Marekani.

Burhanettin Dağ ameashiria kwamba nchi za Ulaya zinapambana kwa njia tofauti na ugonjwa huo na kuongeza kuwa, katika nchi hizo ambazo zimegeuka na kuwa chimbuko la kuenea virusi vya Corona, kumekuwa na habari nyingi za kutisha kuhusiana na kuendelea kuwa mbaya  hali ya kibinaadamu. Mjumbe huo wa Baraza Kuu la Waislamu nchini Ujerumani amesema: "Katika uhalisia wa mambo tunaweza kusema kuwa habari zilizoenea kuhusiana na ugonjwa wa Corona barani Ulaya, ni sehemu ndogo tu ya hali halisi ya mambo."

Burhanettin Dağ, Mjumbe wa Baraza Kuu la Waislamu wa Ujerumani

Kadhalika Burhanettin Dağ ameashiria matamshi ya kugongana ya Rais Donald Trump wa Marekani katika vikao na waandishi wa habari na kusisitiza kuwa, miamala ya kiburi ya rais huyo imegeuka siku za hivi karibuni kuwa maudhui ya kujadiliwa katika vyombo vya habari na kukosolewa pakubwa. Dağ amemalizia kwa kusema kuwa, kuendelea shughuli za maduka ya kuuza silaha za moto nchini Marekani katika hali ya sasa, kunaonyesha hali ya wasi wasi uliopo nchini humo na kwamba sababu yake ni udhaifu wa moyo wa umaanawi na imani.

Maoni