Apr 06, 2020 03:17 UTC
  • Watu 15,887 waaga dunia kwa virusi vya corona huko Italia hadi sasa

Serikali ya Italia jana usiku imetangaza kuwa idadi ya watu walioaga dunia kutokana na mamabukizi ya virusi vya corona nchini humo hadi sasa imefika elfu 15 na 887.

Serikali ya Italia aidha imetangaza maambukizo  mapya  4,316 ya virusi vya ya corona nchini humo katika muda wa masaa 24 yaliyopita; na kueleza kuwa hadi sasa watu 128,947 wameambukizwa virusi vya corona nchini humo. 

Italia inaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya watu walioaga dunia na wale walioambukizwa virusi vya corona kati ya nchi za Ulaya. Giuseppe Conte Waziri Mkuu wa Italia tarehe 10 mwezi Machi mwaka huu alichukua uamuzi wa kuwa chini ya karantini nchi hiyo yenye jumla ya watu milioni sitini kufuatia kuongezeka maambukizo ya corona nchini humo. 

Waziri Mkuu wa Italia, Giuseppe Conte 

Virusi vya corona ambavyo vinafahamika kwa jina rasmi la Covid-19 viligunduliwa kuenea kwa mara ya kwanza mwishoni mwa mwezi Disemba mwaka jana wa 2019 katika mji wa Wuhan mkoan Hubei mashariki mwa China na kisha kuenea katika mikoa 30 ya nchi hiyo. Mamabukizi ya virusi vya corona sasa yameaziathiri nchi zaidi ya 200 duniani zikiwemo Marekani, Italia, Australia, Thailand, Korea ya Kusini, Japan, Canada, Ufaransa, Italia, Uingereza, Uturuki, Saudi Arabia na Imarati. 

 

Maoni