Apr 07, 2020 02:52 UTC
  •  Adams: Wiki hii itakuwa ya masikitiko makubwa kwa Wamarekani sawa na ya Pearl Harbor na Septemba 11 kutokana na vifo vya corona

Mkuu wa Afya wa Serikali ya Federali ya Marekani amesema wiki hii itakuwa "ngumu na ya kusikitisha zaidi" kwa "maisha ya Wamarekani wengi," na amekielezea kipindi kibaya kijacho cha janga la virus vya corona nchini humo kuwa kitakuwa sawa na kile cha "wakati wa mashambulizi ya Bandari ya Pearl Harbor" na "11 Septemba mwaka 2001."

"Wiki hii itakuwa chungu na ya kuhuzunisha sana kama hali ya wakati wa mashambulizi ya Pearl Harbo na 9 Septemba mwaka 2001, lakini mara hii maafa hayo hayatatokea sehemu moja makhsusi bali nchi nzima ya Marekani," amesema Jerome Adams.  

Mkuu huyo wa masuala ya afya wa Serikali ya Federali ya Marekani amewataka wananchi wa nchi hiyo kujitayarisha kwa machungu makubwa watakayokumbana nayo wiki hii kutokana na maafa ya virusi vya corona. 

Wataalamu wa White House wametabiri kuwa Wamarekani baina ya laki moja na laki mbili na arubaini elfu watapoteza maisha kutokana na maambukizi ya virusi ya corona. 

Maiti za Wamarekani walioaga dunia kutokana na corona

Kwa sasa Marekani inashika nafasi ya kwanza duniani kwa kuwa na idadi kubwa zaidi ya waathirika na idadi kubwa zaidi ya watu walioaga dunia kutokana na maambukizi ya corona. Zaidi ya Wamarekani 336,800 wameambukizwa virusi hivyo na karibu elfu 10 miongoni mwao wameaga dunia.

Utendaji mbaya wa serikali na haba wa vifaa na zana za tiba nchini Marekani umeendelea kukosolewa sana na wanasiasa na wananchi wa nchi hiyo, suala ambalo wachambuzi wa mambo wanasema litakuwa na taathira kubwa katika matokeo ya uchaguzi wa rais uliopangwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu. 

Maoni