Apr 07, 2020 23:34 UTC
  • Waziri wa Afya wa Ufaransa atahadharisha kuhusu kufikia kileleni mlipuko wa Corona

Waziri wa Afya wa Ufaransa ametahadharisha kuwa nchi hiyo inakaribia kushuhudia kilele za mlipuko wa virusi vya corona.

Olivier Veran amesema kuwa Ufaransa bado haijafika katika kilele cha maambukizi ya virusi vya corona na kwamba nchi hiyo inaingia katika kipindi baya.  

Taasisi ya Misaada ya Umma ya Hospitali za Paris  (AP-HP) Jumamosi iliyopita ilitabiri kuwa mlipuko wa virusi vya corona ungefikia kileleni katika eneo la " Il de France" siku ya Jumatatu Aprili Sita. Waziri wa Afya wa Ufaransa pia ametangaza kuwa karantini ya nchi nzima kwa ajili ya kukabiliana na corona itaendelea iwapo italazimu. 

Siku ya Jumatatu wiki hii pia Waziri huyo wa Afya wa Ufaransa alikuwa ametahadharisha kuwa maambukizo ya virusi vya corona nchini humo yangali yanaongezeka kwa kasi na kwamba idadi kubwa ya wagonjwa wenye maambukizi, walioga dunia na wale waliolazwa katika vitengo vya wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu inabainisha hali halisi ya mambo. 

Wagonjwa mahututi wa corona nchini Ufaransa 

Takwimu za Wizara ya Afya ya Ufaransa zinaonyesha kuwa, jumla ya watu 29,722 wamelazwa hospitalini kutokana na maambukizi ya corona na wagonjwa 7,072 miongoni mwao wamelazwa katika vitengo vya wagonjwa mahututi. Aidha watu 8,911 wameaga dunia hadi sasa nchini Ufaransa. Jumla ya watu wasiopungua 98,010 wameambukizwa virusi vya corona nchini humo

Tags

Maoni