Apr 09, 2020 02:42 UTC
  • Mgogoro wa Corona na sisitizo la viongozi wa Russia la kufutwa vikwazo

Naibu Mkuu wa Baraza la Federesheni ya Russia amesisitizia udharura wa kufutwa vikwazo duniani kwa lengo la kukabiliana na tishio la Corona.

Dmitry Medvedev, Naibu Mkuu wa Baraza la Federesheni ambaye pia ni waziri mkuu wa zamani wa nchi hiyo amesema kuwa, kwa kuzingatia mgogoro wa sasa unaotokana na Corona hii leo, dunia inahitaji kuwa na uhusiano mpya ulio mbali na vikwazo na utakaosimama juu ya msingi wa wa nchi zote kusaidiana. Medvedev amebainisha kuwa, hivi sasa ambapo virusi vya Corona vinaenea kwa kasi kubwa duniani, na hivyo kupelekea ulimwengu kumbwa na mgogoro mkubwa, nchi zote zinatakiwa kufanya juhudi maalum za kushirikiana na  kusaidiana.

Dmitry Medvedev, Naibu Mkuu wa Baraza la Federesheni ya Russia

Ameweka wazi kuwa, katika kukabiliana na tishio hilo hatari, dunia inapaswa kutokuwa na vikwazo. Wiki kadhaa zilizopita, viongozi wa Russia walikosoa mara kadhaa vikwazo vya upande mmoja vya Marekani dhidi ya nchi nyingine, hususan zile ambazo zinakumbwa na mgogoro wa virusi vya Corona. Pamoja na hayo serikali ya Marekani haijatoa jibu lolote kuhusu matakwa ya walimwengu ya kupunguziwa vikwazo nchi kama vile Iran na Cuba. 

Tags

Maoni