Apr 10, 2020 08:19 UTC
  • Oxfam: Virusi vya corona vitawatumbukiza watu milioni 500 katika janga la umaskini

Shirika la kimataifa la misaada ya kibinadamu la Oxfam limetahadharisha kuwa athari mbaya za kiuchumi zilizosababishwa na mlipuko wa virusi vya corona zinaweza kuwatumbukiza watu milioni 500 katika njanga la umaskini.

Ripoti iliyotolewa na Oxfam imesema kuwa, zaidi ya watu nusu bilioni moja watatumbukia katika umaskini iwapo hatua za haraka za kuzisaidia nchi maskini zilizoathiriwa na maambukizi ya virusi vya corona hazitachukuliwa.

Taarifa hiyo imesema kuwa athari za kufungwa taasisi za kiuchumi katika jitihada za kupambana na maambukizi ya virusi vya corona zinahatarisha kurejesha nyuma kwa miongo kadhaa mapambano dhidi ya umaskini katika nchi zinazostawi, na asilimia 6 hadi 8 ya jamii ya dunia itatumbukia katika umaskini.

Ripoti hiyo imeongeza kuwa nusu na nafasi za kazi na ajiri zote barani Afrika zitatoweka kutokana na athari mbaya za virusi vya corona kama hatua za haraka hazitachukuliwa.

Oxfam: Watu nusu bilioni watatumbukia katika umaskini kutokana na maambukizi ya corona

Ripoti ya Oxfam imechapishwa kabla ya mikutano ya kawaida ya mawaziri wa kifedha wa kundi la G20 la mataifa yaliyoendelea na yanayoendelea, Mfuko wa Fedha wa Kimataifa na Benki ya Dunia. 

Zaidi ya watu 1,605,683 wameambukizwa virusi vya corona kote duniani na karibu laki moja wameaga dunia kutokana na ugonjwa huo. 

Tags

Maoni