Apr 10, 2020 08:20 UTC
  • Viongozi wa dini duniani watoa wito wa kufutwa vikwazo vya Marekani dhidi ya Iran

Viongozi wa dini jana Alkhamisi walimwandikia barua Rais Donald Trump wa Marekani wakimtaka aondoe vikwazo vya nchi hiyo dhidi ya Iran.

Muungano wa ACT unaoundwa na zaidi ya makanisa na jumuiya 145 za makanisa katika zaidi ya nchi 120 duniani, Baraza la Kimataifa la Makanisa na Baraza la Kitaifa la Makanisa ya Kikristo yamesisitiza katika barua hiyo ya pamoja udharura wa kuondolewa vikwazo vilivyowekwa dhidi ya Iran hususan katika kipindi hiki cha mgogoro wa virusi vya corona.

Barua hiyo ya viongozi wa makanisa ya nchi zaidi ya 120 imevitaja virusi vya corona kuwa ni adui wa pamoja wa wanadamu wote na kwamba suala la kupambana na virusi hivyo linahitajia ushirikiano mkubwa wa duniani, kuwashughulikia zaidi watu wanaokabiliwa na hatari kubwa na kuchukua hatua za haraka za kuondoa mazingira yanayaoweza kusababisha madhara makubwa zaidi.

Donald Trump

Viongozi wa kidini duniani wamesema katika barua hiyo kwamba, wana wasiwasi kuhusu taathira mbaya za vikwazo vya Marekani kwa maisha ya raia wa kawaida wa Iran na kuongeza kuwa: Vikwazo vya upande mmoja vya Marekani dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu vinatatiza mapambano ya Tehran ya kuangamiza virusi vya corona. 

Vikwazo hivyo vya kidhalimu vya Marekani ambavyo vinajumuisha hata bidhaa muhimu zikiwemo dawa na vifaa vya tiba, vinawasababishia matatizo watu wa Iran hususan katika kipindi cha sasa cha mapambano dhidi ya virusi vya corona.    

Maoni