May 21, 2020 08:08 UTC

Kwa uchache watu 11 wamejeruhiwa baada ya gari moja kuvamia kwa makusudi duka moja la nguo za staha ya mwanamke Muislamu yaani Hijab huko Greenacre, New South Wales, Australia. Dereva wa gari hiyo amegonga gari nyingine kabla ya kukanyaga mafuta kwa nguvu zote na kuipigiza gari hiyo na duka hilo la Hijab.

Shirika la habari la RT la Russia limeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, kwa uchache watu 11 wamejeruhiwa baada ya gari moja kuvamia kwa makusudi duka moja la nguo za staha ya mwanamke Muislamu yaani Hijab huko Greenacre, New South Wales, Australia. Dereva wa gari hiyo amegonga gari nyingine kabla ya kukanyaga mafuta kwa nguvu zote na kuipigiza gari hiyo na duka hilo la Hijab.

Polisi wamefika haraka kwenye sehemu hiyo baada ya kusikia ripoti kuwa, kuna dereva mmoja anafanya vitendo vya kiwendawazimu kwenye eneo hilo. Hata hivyo walipofika dereva huyo alishalipigisha gari na duka hilo la mavazi ya staha ya Waislamu (Hijab).

Dereva wa gari hiyo mwenye umri wa miaka 51 pamoja na wapita njia 11 wamejeruhiwa. Polisi wamesema, majeraha ya majeruhi hao si ya kutisha.

Maoni