May 22, 2020 02:42 UTC
  • Majeshi ya Pakistan na India yashambuliana katika mstari wa udhibiti

Kufuatia mashambulizi ya mizinga yaliyotekelezwa na askari wa mpakani wa India katika mstari wa udhibiti katika eneo la Kashmir katika ardhi ya Pakistan, raia watatu wa nchi hiyo wamejeruhiwa.

Jeshi la Pakistan limetangaza kwamba askari wake wa kulinda mpaka wamejibu mashambulizi ya mizinga yaliyotekelezwa na askari wa mpakani wa India na kuwasababishia hasara kubwa askari hao wa nchi jirani. Sambamba na kulaani hujuma za ukiukaji wa makubaliano ya usitishaji vita katika mstari wa udhibiti eneo la Kashmir zinazofanywa na askari hao wa mpakani wa India, jeshi la Pakistan limesema kuwa tangu ulipoanza mwaka huu wa 2020 hadi sasa, askari wa kulinda mpaka wa nchi hiyo jirani wamekiukaji mapatano ya usitishaji vita zaidi ya mara 100. Aidha Wizara ya Mambo ya Nje ya Pakistan katika malalamiko yake kuhusiana na hujuma za askari wa India dhidi ya raia wa kawaida wa Pakistan, imemwita mwanadiplomasia wa ngazi ya juu wa ubalozi wa India nchini humo na kumfikishia malalamiko yake hayo.

Askari wa mpakani wa India na Pakistan

India na Pakistan zina tofautiana katika masuala mengi likiwemo suala la eneo la Kashmir ambapo kila moja inamtuhumu mwenzake kwa kukiuka makubaliano ya usitishaji vita na kufanya vitendo vya kigaidi. Katika uwanja huo, sambamba na kushadidi mapigano ya mpakani kati ya nchi hizo, kwa mara nyingine Waziri Mkuu wa Pakistan, Imran Khan ameitahadharisha India kwa kile alichosema ni operesheni bandia za nchi hiyo. Imran Khan aliyasema hayo jana Alkhamisi ambapo sambamba na kukosoa mienendo ya serikali ya New Delhi katika eneo la Kashmir lililo chini ya udhibiti wa India na pia ukandamizaji dhidi ya waandamanaji wa eneo hilo, ameitaka jamii ya kimataifa kuilazimisha India ihitimishe mashambulizi yake dhidi ya Waislamu wa eneo hilo