May 22, 2020 02:42 UTC
  • Russia yakanusha kuwepo mvutano katika uhusiano wake na Syria

Balozi wa Russia nchini Syria ametupilia mbali madai ya kuwepo hitilafu katika uhusiano wa serikali ya Moscow na Damascus.

Aleksandr Yefimov amekadhibisha suala la kuwepo aina yoyote ya hitilafu kati ya nchi mbili na kusisitiza kwamba, maadui wanatumia kila wenzo kwa ajili ya kuibua tofauti kati ya nchi hizo. Yefimov ameongeza kwamba, madai yanayotolewa kwamba kuna tofauti katika uhusiano wa Russia na Syria ni uongo mtupu na hayana ukweli wowote. Aidha balozi huyo wa Russia nchini Syria amesisitiza kwamba uhusiano uliopo kati ya nchi yake na Syria ni ni imara, wa kirafiki na kistratijia zaidi kuliko wakati mwingine wowote ule.

Aleksandr Yefimov, Balozi wa Russia nchini Syria 

Russia imekuwa na nafasi muhimu katika harakati za mapambano dhidi ya ugaidi nchini Syria na daima imekuwa ikisisitizia juu ya ulazima wa kuheshimiwa haki ya raia wa nchi hiyo kujiamulia mustakbali wao bila ya uingiliaji wowote wa kigeni. Katika miezi ya hivi karibuni vyombo vya habari vya Magharibi vimekuwa vikieneza habari za uongo za kuwepo hitilafu kubwa katika uhusiano wa Russia na Syria na kudai kwamba serikali ya Moscow inamtaka Rais Bashar Al-Assad wa nchi hiyo aondoke madarakani.

Tags