May 22, 2020 02:43 UTC
  • Trump na Nancy Pelosi washambuliana vikali kwa maneno

Kwa mara nyingine Rais Doanald Trump wa Marekani ameshambuliana vikali kwa maneno na Nancy Pelosi, Spika la Bunge la Wawakilishi la nchi hiyo.

Katika mahojiano na kanali ya televisheni ya MSNBC Pelosi amemlinganisha Trump na mtoto aliyevaa viatu vilivyotapakaa kinyesi cha mbwa. Akitoa radiamali kuhusiana na matamshi ya Trump spika huyo wa bunge la wawakilishi  la Marekani amesema kuwa rais huyo wa Marekani ataendelea kuwa sawa na mtoto ambaye amevaa suruali iliyochafuka kwa na matope. Kabla ya hapo pia Nancy Pelosi alimkosoa Trump kutokana na maneno yake juu ya matumizi ya kidonge kimoja cha Hydroxychloroquine kila siku kwa ajili ya kuzuia maambukizi ya virusi vya Corona na kusema kuwa, kutokana na rais huyo kuwa mwenye umri mkubwa na mnene wa kupindukia, hapaswi kutumia dawa hiyo.

Trump na Nancy Pelosi ambao hawaelewani

Katika radiamali yake dhidi ya Pelosi, Trump amemtaja spika huyo wa bunge la wawakilishi kuwa ni mwanamke mgonjwa na mwenye matatizo mengi. Ushauri wa Trump wa kutumia dawa ya Hydroxychloroquine kwa mara nyingine umeibua ukosoaji mkali katika vyombo vya habari dhidi ya rais huyo. Ni miezi kadhaa sasa ambapo Trump na Pelosi wamekuwa wakishambuliana kwa maneno moja kwa moja, mashambulio ambayo yameongezeka ndani ya wiki hii.

Tags