May 22, 2020 11:31 UTC
  • Taasisi ya kijamii ya Italia: Idadi kamili ya wahanga wa firusi vya Corona ni zaidi ya iliyotangazwa

Taasisi ya Usalama wa Kijamii nchini Italia imesema kuwa, idadi kamili ya watu waliopoteza maisha kutokana na virusi vya Corona kati ya mwezi Machi na Aprili mwaka huu ni zaidi ya watu elfu 19 waliotangazwa rasmi na serikali.

Taasisi hiyo ya Italia yenye uhusiano na idara ya usalama wa kijamii ya nchi hiyo imesema kwamba, watu laki moja na elfu 56,429 walifariki dunia kati ya mwezi Machi na Aprili mwaka huu nchini humo kutokana na sababu tofauti zikiwemo za virusi hatari vya Corona. Kwa mujibu wa taasisi hiyo ya kitaifa ya bima ya kijamii nchini Italia, viongozi wa serikali wametangaza idadi ya watu waliofariki dunia kwa virusi vya Corona nchini humo kuwa ni elfu 19, katika hali ambayo karibu watu elfu 50 wamepoteza maisha kwa virusi hivyo ndani ya nchi hiyo.

Virusi vya Corona ndani ya nchi za Ulaya

Hii ni katika hali ambayo katika kipindi hicho viongozi wa serikali ya Italia walitangaza idadi ya vifo zaidi ya elfu 32 kutokana na sababu zingine mbali na virusi. Aidha idadi kamili ya watu waliopoteza maisha nchini humo ndani ya mwezi Machi na Aprili jati ya mwaka 2015 na 2019 ilipungua kwa watu elfu 50.

Tags

Maoni