May 24, 2020 02:51 UTC
  • Uingereza yachukizwa na hotuba ya Kiongozi Muadhamu ya kuitetea Palestina

Hotuba ya kistratijia na ya kutia matumaini ya Kiongozi Muadhamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei katika kuitetea Palestina na kufichua njama chafu za utawala haramu wa Kizayuni wa Israel na waungaji mkono wake, imewatia hasira viongozi wa Uingereza.

Dominic Raab, Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza ameandika kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter kuhusiana na hotuba ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu aliyoitoa siku ya Ijumaa kwa mnasaba wa Siku ya Kimataifa ya Quds; na bila kuashiria uungaji mkono wa moja kwa moja na usio wa moja kwa moja wa serikali ya London kwa utawala haramu wa Kizayuni, waziri huyo wa mambo ya nje wa Uingereza amedai kwamba hotuba ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu inawalenga Wayahudi na kwamba haikubaliki.

Dominic Raab, Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza

Badala ya Dominic Raab kuzungumzia suala la kukanyagwa haki za kibinaadamu za watu wa Palestina kwa makumi ya miaka, amedai kwamba haki ya amani na usalama ya utawala haramu wa Israel ni jambo lisilopingika na kwamba kupuuzwa jambo hilo kunawachukiza watu wote wa eneo. Itakumbukwa kuwa Ijumaa Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu alitoa hotuba kwa mnasaba wa Siku ya Kimataifa ya Quds ambapo sambamba na kuashiria kuingia kipindi kipya cha mapambano ya Wapalestina baada ya Ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu na kudhihiri mrengo wa muqawama sambamba na kubadilika mlingano wa nguvu kwa maslahi ya wanamuqawama, alitoa miongozo saba muhimu kuhusiana na kuendelezwa jihadi kubwa na tukufu ya hivi sasa.

 

Tags

Maoni