May 24, 2020 02:52 UTC
  • Mtengeneza filamu wa Marekani: Trump atashinda tu iwapo kutafanyika uchakachuji katika uchaguzi

Mtengeneza filamu mashuhuri wa nchini Marekani amebainisha kwamba, njia pekee inayoweza kumfanya Rais Donald Trump wa nchi hiyo aibuke mshindi katika uchaguzi ujao ni uchakachuaji.

Michael Moore, muelekezi na mtengeneza filamu maarufu wa Marekani ambaye pia ni mkosoaji mkubwa wa Trump amesema kuwa, rais huyo hana nafasi yoyote ya kuweza kushinda uchaguzi ujao nchini humo, labda tu afanye ufanganyifu. Aidha amezungumzia miamala ya serikali ya Trump katika kipindi cha kuenea virusi hatari vya Corona na kuongeza kwamba utendaji wa Trump katika suala hilo ni wenye kukosolewa vikali na ni kwa ajili hiyo ndio maana umaarufu wake ukapungua sana.

Michael Moore, mtengeneza filamu mashuhuri wa Marekani 

Muelekezi na mtengeneza filamu huyo wa Marekani  amesema kuwa, njia pekee iliyobaki mbele ya Trump ni ima kususia, kufuta au kuahirisha uchaguzi ujao. Ni vyema kuashiaria kwamba hatua na misimamo ya Trump kuhusiana na kuenea kwa virusi vya Corona nchini Marekani, imekuwa iikikosolewa vikali. Katika uwanja huo, Joe Biden, mpinzani wa Trump kutoka chama cha Democrat kwenye uchaguzi wa Novemba mwaka huu nchini Marekani, ameonekana kumbwaga rais huyo kwenye uchunguzi mpya wa maoni uliofanyika hivi karibuni.

Tags

Maoni