May 25, 2020 06:41 UTC
  • Rais Tayyip Erdoğan: Quds ni mstari mwekundu wa Waislamu duniani

Rais Recep Tayyip Erdoğan wa Uturuki amesema katika ujumbe alioutoa kwa mansaba wa Idul-Fitr kwamba, Quds ni mstari mwekundu wa Waislamu duniani.

Aidha Rais Erdoğan sambamba na kukosoa mpango wa utawala haramu wa Kizayuni wa kuyaunganisha maeneo ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu (Israel) amesema kuwa, Uturuki haitokubali uvamizi wowote wa ardhi za Wapalestina. Sambamba na kubainisha kwamba utawala haramu wa Israel kupitia uvamizi wa ardhi za Wapalestina umepuuza haki za Wapalestina na za kimataifa, amekosoa vikali hatua kandamizi za wavamizi wa Kizayuni.

Quds, kibla cha kwanza cha Waislamu duniani

Hivi karibuni Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala bandia wa Kizayuni alitangaza kwamba mpango wa kuyaunganisha maeneo ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na utawala huo, utatekelezwa katika miezi michache ijayo. Suala hilo ni moja ya vipengee vya muamala wa kibaguzi wa karne ambao aliuzindua Rais Donald Trump wa Marekani tarehe 28 Januari mwaka huu. Muamala wa Karne, ni mpango mpya uliobuniwa na serikali ya Marekani kwa ushirikiano wa baadhi ya nchi vibaraka za Kiarabu ikiwemo Saudia kwa lengo la kuendelea kukanyaga haki za raia madhlumu wa Palestina. Nchi nyingi, shakhsia, viongozi wa kisiasa na kidini kote duniani hususan Waislamu, wamelaani vikali mpango huo wa kibaguzi.

Maoni