May 25, 2020 07:01 UTC
  • Kim Jong-un, aongoza kikao cha nyuklia mjini Pyongyang, Korea Kaskazini

Kikao cha kuchunguza ongezeko la uwezo wa kijeshi na silaha za nyuklia za Korea Kaskazini, kilifanyika Jumapili ya jana kwa kuhudhuriwa na Kim Jong-un, Kiongozi wa nchi hiyo mjini Pyongyang.

Vyombo vya habari vya Korea Kaskazini vimeripoti kwamba katika kikao hicho kulijadiliwa mwenendo wa kuimarishwa uwezo wa jeshi la nchi hiyo dhidi ya vitisho vya kijeshi vinavyoikabili nchi hiyo. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, kuimarishwa siasa za kujilinda kijeshi katika uga wa nyuklia wa Korea Kaskazini na kuandaliwa stratijia ya kujiweka tayari kikamilifu jeshi la nchi hiyo, ni maudhui nyingine zilizojadiliwa katika kikao hicho. Aidha kikao hicho kiliamua kuzidisha uwezo wa vikosi vya mizinga nchini Korea Kaskazini.

Ukwamishaji mambo wa Marekani, ndio sababu ya Korea Kaskazini kuinua uwezo wake wa silaha za nyuklia

Kikao cha kuongezwa uwezo wa kijeshi na nyuklia mjini Pyongyang, kimefanyika baada ya kusimama mazungumzo ya Washington na Pyongyang kwa lengo la kuangamizwa silaha za nyuklia za Korea Kaskazini. Hata hivyo ukwamishaji mambo wa Marekani na kushindwa kuifutia vikwazo Korea Kaskazini na pia sisitizo lake la kuendelea kufanya maneva ya kijeshi kwa kushirikiana na Japan na Korea Kusini katika Rasi ya Korea, kulipelekea kusimama mazungumzo hayo ya pande mbili.

Tags

Maoni