May 25, 2020 07:08 UTC
  • Corona na maandamano dhidi ya Trump katika jimbo la Virginia

Wakazi wa jimbo la Virginia nchini Marekani wamefanya maandamano mbele ya kilabu ya Trump katika jimbo hilo, wakilalamikia uongozi wake mbovu katika mapambano dhidi ya virusi vya Corona.

Waandamanaji hao waliokuwa wamebeba mabango yaliyokuwa na maandishi yenye maneno yanayosema 'acheni kutuua' wamelaani vikali uongozi mbovu wa Trump kuhusu makabiliano ya serikali yake na virusi hivyo. Hivi sasa Trump na serikali yake kwa ujumla wanakosolewa vikali kutokana na usimamizi mbaya kwenye mapambano ya virusi vya Corona nchini Marekani.

Serikali ya Trump imeshindwa kukabiliana na virusi vya Corona

Hadi sasa Marekani inaongoza duniani kwa kuwa na idadi kubwa ya waathirika na wahanga wa ugonjwa wa Covid-19 unaosababishwa na virusi vya Corona. Kwa mujibu wa takwimu mpya, idadi ya waathirika wa virusi vya Corona nchini humo imefikia milioni moja na laki 6 na elfu 67,437, huku idadi ya waliopoteza maisha ikiwa ni elfu 99,300.

Tags

Maoni