May 25, 2020 07:15 UTC
  • Rais Nicolás Maduro wa Venezuela aishukuru Jamhuri ya Kiislamu ya Iran

Rais Nicolás Maduro wa Venezuela ameshukuru uungaji mkono wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa serikali na watu wa nchi hiyo.

Rais Maduro aliyasema hayo jana usiku ambapo akiashiria kuwasili meli ya kwanza ya Iran iliyobeba mafuta katika pwani ya Venezuela na sambamba na kuishukuru serikali na watu wa Iran alisema kuwa, Venezuela haipo peke yake bali ina marafiki mashujaa ambao wamesimama pamoja na serikali ya Caracas. Rais huyo wa Venezuela ambaye alikutana na wajumbe wa kamati ya rais ya kupambana na virusi vya Corona amesisitiza kwamba Iran na Venezuela zinataka amani na kuongeza kwamba nchi mbili zinayo haki ya kufanya biashara katika maji ya kimataifa kwa uhuru kamili.

Meli za mafuta za Iran zikiwa safarini kuelekea Venezuela

Kadhalika Rais Nicolás Maduro ameandika katika mtandao wa kijamii wa Twitter akiishukuru Iran kwa hatua yake ya kuitumia nchi yake mafuta ambapo akiambatanisha na picha ya meli ya mafuta ya Iran inayoitwa 'Fortune' amesema: "Kumalizika kwa mwezi wa Ramadhani kumetuletea matukufu kwa kuwasili meli ya Fortune." Kadhalika ameongeza kuwa, katika hali ambayo nchi za kibeberu zinataka kuyatwisha mataifa mangine mabavu yao, ni udugu tu ndio unaoweza kuwaokoa watu walio huru. Inafaa kuashiria kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na katika fremu ya kuunga mkono serikali na watu wa Venezuela ambao wako chini ya mzingiro wa kiuchumi wa Marekani, imetuma meli tano zilizobeba mafuta kuelekea nchi hiyo ya Amerika ya Latini. Meli ya kwanza kwa jina la Fortune iliwasili jana katika bandari ya Venezuela. Aidha meli ya pili nayo imeingia katika maji ya Venezuela, huku meli zingine tatu zikiwa bado safarini kuelekea nchi hiyo.

Maoni