May 25, 2020 10:31 UTC
  • Sisitizo la Venezeula kuhusu kutokuwa na maana vitisho vya Marekani dhidi ya meli za mafuta za Iran

Wakati wa utawla wa rais Donald Trump wa Marekani, sera za mashinikizo ya pande zote dhidiya Venezeula zimeongezeka kwa kuwekewe vikwazo vingi nchi hiyo lengo likiwa ni kuipindua serikali ya Rais Nicolas Maduro na kumleta madarakani kinara wa wapinzani Juan Guaid ambaye ni kibaraka wa Washington.

Mkabala wa sera hizo, waitifaki wa Venezuela, ikiwemo Iran, wamekuwa wakifuatilia sera za kuisaidia nchi ya Amerika ya Kusini kusimama kidete mbele ya ubabe wa Washington.

Pamoja na kuwa Venezuela ina utajiri mkubwa wa mafuta ghafi ya petroli lakini viwanda vyake vya kusafisha mafuta havifanyi kazi kutokana na vikwazo vya Marekani. Viongozi wa Marekani wanadai kwamba mauzo ya mafuta ya Iran kwa Venezuela ni kinyume cha sheria na kwamba ni lazima wakabiliane na suala hilo. Ni kwa msingi huo ndipo wakatuma askari wa baharini wa Marekani karibu na maji ya Venezuela.

Kutumwa meli tano za mafuta za Iran ambazo zimebeba mafuta kwa ajili ya Venezuela ni hatua ambayo imekumbwa na uhasama wa utawala wa Trump ambapo ameamuru jeshi la Marekani litume manoari zake kwa lengo la kuitisha Iran ili kusitishe safari za meli hizo. Pamoja na kuwepo vitisho hivyo, Iran haijatishika na meli zake hizo za mafuta zimeendelea na safari  ya kuelekea Venezuela na tayari meli moja imeshatia nanga katika bandari ya nchi hiyo  na ya pili tayari imeshaingia katika maji ya Venezuela.

Hatua hiyo ni ya kihistoria katika kuvunja sera za mashinikizo ya juu kabisa ya Marekani dhidi ya Iran na Venezuela.

Balozi wa  Venezuela katika Umoja wa Mataifa Samuel Moncada ameandika ujumbe katika ukurasa wake wa Twitter na kusema: “Kufika petroli ya Iran kwa ajili ya watu wa Venezuela ni nukta muhimu katika mapambano ya kuwa na mamlaka ya kujitawala, uhuru na amani. Trump na watumwa wake walikuwa wanatafakari kuhusu kushambulia kijeshi meli hizi katika wakati huu wa  janga la COVID-19 lakini ameshauriwa vingine na wataalamu.”

Meli ya mafuta ya Iran ikielekea Venezuela ikiwa imesindikizwa na manoari ya Jeshi la Venezuela

Kwa mujibu wa taarifa katika vyombo vya habari vya Venezuela, meli ya Iran inayosheheni petroli ijulikanayo kama Fortune, ilisindikizwa na Jeshi la Majini la Venezeula na Jumapili ilitia nanga katika bandari ya El Palito kaskazini mwa pwania ya nchi hiyo.

Ubalozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Venezuela umeandika ujumbe katika Twitter na kusema: “Leo zaidi ya wakati wowote ule, mshikamano wa kirafiki na kidugu baina ya Iran na Venezuela umepata nguvu na umeimarika. Meli ya kwanza imewasili. Tunalishukuru Jeshi la Majiini la Venezuela kwa kuisindikiza. Uhusiano wa kiraifiki wa Iran na Venezuela uendelee kuwa hai.”

Hatua ya Iran kutuma meli zake zinazosheheni petroli nchini Venezuela ni jambo ambalo limewakasirisha sana wakuu wa Marekani kiasi kwamba Washington ilikuwa imeapa kuwa itazuia meli hizo za Iran kufikisha petrol Venezuela. Ni kwa msingi huo ndio katika siku za hivi karibuni kumekuwepo na tetesi katika vyombo vya habari vya Kimagharibi  kuwa meli  hizo tano, ambazo zimeenda Venezuela kufuatia ombi la nchi hiyo, zitasimamishwa katika maji ya kimataifa.

Pamoja na hayo, Iran imeonyesha msimamo imara na ikaionya Marekani kuwa isithubutu kuchukua hatua yoyote ya uchokozi wa kijeshi dhidi ya meli hizo kwani ikifanya hivyo itakabiliwa na jibbu kali la Iran. Onyo hilo la Iran limepelekea Trump asitishe vitisho vyake vya awali. Wakati kuliposambazwa taarifa kuhusu kuongezeka idadi ya manaori za Jeshi la Majini la Marekani katika Bahari ya Caribbean, Mohammad Javad Zarif Waziri wa Mambo ya Nje ya Iran alimtumia barua Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres na kumuarifu kuhusu chokochoko hizo za Marekani. Zarif alimfahamisha Guterres kuwa kuna uwezekano wa Marekani kuzihujumu meli za Iran zinazotuma mafuta nchini Venezuela. Iran ilitahadahrisha kuwa, uchokozi wowote dhidi ya meli za mafuta za Iran utakabiliwa na jibu.

Rais Hassan Rouhani wa Iran (kushoto) na Rais Nicolas Maduro wa Venezuela

Naye Rais Hassan Rouhani wa Iran katika mazungumzo ya simu ya Emir wa Qatar alisema kuwa, iwapo meli za Iran zitachokozwa na Marekani katika Bahari ya Caribbean, Iran nayo itajibu uchukozi huo.

Kitendo cha Iran kutuma meli zilizojaa mafuta nchini Venezuela ni jambo linaloashiria mshikamano wa nchi hizi mbili na ni nembo ya mapambano ya nchi hizi mbili katika kukabiliana na vitisho na njama za Marekani. Katika upande wa pili kadhia hii inayonyesha kuwa, sera za Marekani za kuangusha serikali za Iran na Venezuela zimefeli kabisa na vitisho vya Trump  havina  taathira kwa nchi hizi mbili zipingazo ubabe wa Washington. Jambo hili limewatia wasi wasi mkubwa wanasiasa wenye misimamo mikali na ya kufurutu ada nchini Marekani.

John Bolton, mshauri wa zamani wa usalama wa taifa nchini Marekani ameashiria kuingia meli za mafuta za Iran katika Bahari ya Carribean na kufikishwa mafuta ya Iran nchini Venezuela na kusema: “Hatua hii ni hatari kwa Markeani kwani katika kupinga ushawishi wa Iran, Washingotn ilisimama pamoja na Juan Guaido.

Pamoja na kuwepo vitisho vya Marekani, Jamhuri ya Kiislamu imesimama kidete katika uhusiano na waitifaki wake ikiwemo Venezuela na wala haiogopi vitisho vya wakuu wa Marekani.

 

Tags

Maoni