May 31, 2020 04:22 UTC
  • Cuba na Venezuala zalaani ukatili wa polisi wa Marekani dhidi ya watu weusi

Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Cuba na Venezula wamelaani vikali ukatili wa polisi wa Marekani dhidi ya Wamarekani weusi pamoja na ujumbe wa kuchochea utumiaji mabavu alioutoa Rais Donald Trump.

Bruno Rodríguez, Waziri wa Mambo ya Nje wa Cuba sambamba na kulaani mauaji ya kutisha ya Mmarekani mweusi yaliyotekelezwa na polisi mzungu wa nchi hiyo, ameandika kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter kwamba 'George Floyd hajafariki dunia.' Katika ujumbe huo Rodríguez ameongeza kwamba; "Floyd ameuawa kwa njia ya kutisha na jambo la kusikitisha ni kwamba jinai hizo zimezoeleka dhidi ya Wamarekani wenye asili ya Afrika." Naye Jorge Arreaza, Waziri wa Mambo ya Nje wa Venezuela sambamba na kulaani ujumbe wa Rais Donald Trump wa Marekani kufuatia mauaji ya Floyd amesema kuwa hayo ni matokeo ya kufuata falsafa ya ukatili.

Bruno Rodríguez, Waziri wa Mambo ya Nje wa Cuba, (kulia) na Jorge Arreaza, Waziri wa Mambo ya Nje wa Venezuela kkushoto

Awali Trump alitoa vitisho kwamba iwapo maandamano ya watu weusi ya kulaani ukatili wa polisi yataendelea, basi maafisa wa usalama watawafyatulia risasi. Aidha katika ujumbe huo rais huyo wa Marekani amewataja waandamanaji hao kuwa ni wahuni na waibua ghasia. Maandamano ya wananchi yaliibuka baada ya kuuawa kikatili na polisi mzungu, George Floyd siku ya Jumatatu jioni ambapo maandamano hayo bado yanaendelea hadi sasa. Kufuatia maandamano hayo ikulu ya White House imesitisha shughuli zake kwa muda.

Tags

Maoni