Jun 01, 2020 17:19 UTC
  • Sisitizo la Marekani la kuendelea kuwepo kijeshi nchini Afghanistan

Mwakilishi wa kudumu wa Marekani katika Muungano wa Kijeshi wa Nchi za Magharibi (NATO) amesisitizia kuendelea kuwepo askari wa nchi yake nchini Afghanistan.

Ki Billi Hutcheson ametupilia mbali ripoti ya hivi karibuni ya vyombo vya habari kuhusu juhudi za Rais Donald Trump za kutaka kuondoa askari wa nchi yake kutoka Afghanistan kabla ya kufanyika uchaguzi wa rais wa mwezi Novemba na ameweka wazi kwamba, mpango huo hauko katika vipaumbele vya Washington. Matamshi ya mwakilishi wa Marekani katika Muungano wa Kijeshi wa Nchi za Magharibi (NATO) kwamba nchi yake haina mpango wowote wa kuondoa askari wake kutoka Afghanistan, ni ishara ya wazi ya kutofungamana Washington na ahadi zake juu ya suala la kuondoa askari wake na kuhitimisha vita na ukatili nchini Afghanistan. Serikali ya Marekani na wakati wa kutiwa saini makubaliano ya amani ya tarehe 29 Februari mwaka huu huko Doha, Qatar iliahidi kwamba itawaondoa askari wake kikamilifu kutoka Afghanistan.

Askari wa Marekani nchini Afghanistan akilia mithili ya mtoto baada ya kukumbwa na shambulizi

Licha ya kupita miezi kadhaa tangu kutiwa saini makubaliano hayo, serikali ya Washington haijaweka wazi tarehe ya kuondoka askari wake kutoka taifa hilo la Asia. Sambamba na mwakilishi wa Marekani ndani ya NATO kukiri kwamba nchi yake haina mpango wa kuondoka Afghanistan, inaonekana kwamba utekelezwaji wa makubaliano ya amani ya nchi hiyo kuhusu suala la kuondoa askari wake kutoka Afghanistan, utakumbwa na matatizo. inapaswa pia kufahamika kwamba iwapo Marekani itakiuka ahadi yake ya kuondoa askari wake nchini Afghanistan, mwenendo ulioanza wa amani ya nchi hiyo utarejea nyuma kwenye zama za kabla ya makubaliano ya Doha, ambapo kwa mara nyingine tena Afghanistan itageuka na kuwa uwanja wa ghasia na ukatili. Katika mazingira hayo, hata matumaini ya kufanyika mazungumzo kati ya Waafghani pia yatasambaratika sambamba na kusimama mwenendo wa kudai usalama na amani wa raia wa nchi hiyo kutokana na siasa za hadaa na za upande mmoja za Marekani. Kwa kuzingatia kuibuka baadhi ya viashiria kuhusiana na kulainika misimamo ya kundi la Taleban katika wiki za hivi karibuni ikiwemo usitishaji vita wa siku tatu kwa mnasaba wa Sikukuu ya Idul-Fitri na katika fremu ya kuandaa mazingira ya kufanyika mazungumzo kati ya Waafghani, hivyo kuvunjika kwa mwenendo wa juhudi za sasa nchini humo kwa ajili ya kuhitimisha vita utategemea utekelezaji ahadi wa Marekani.

Ki Billi Hutcheson, Mwakilishi wa kudumu wa Marekani katika Muungano wa Kijeshi wa Nchi za Magharibi (NATO)

Ambapo kinyume na utekelezaji ahadi wa kuondoa askari wake kutoka Afghanistan si tu kwamba Washington haijaainisha muda rasmi wa kuondoa askari hao, bali kwa mujibu wa mwakilishi wa Marekani katika Muungano wa Kijeshi wa Nchi za Magharibi (NATO), Marekani haina nia kabisa ya kuondoka kutoka nchi hiyo. Mtazamo huo unadhihiri ambapo Marekani na kwa kisingizio cha kupambana na magaidi wa Daesh (ISIS) inafanya njama pia za kuhalalisha uwepo wake kijeshi ndani ya taifa hilo licha ya kutia saini makubaliano ya amani ya mjini Doha, Qatar. Kuhusiana na suala hilo, Javid Kuhestani mtaalamu wa masuala ya kijeshi wa Afghanistan anasema kwamba: "Washington na kwa kisingizio cha Daesh (ISIS) inataka kuhalalisha uwepo wake kijeshi nchini Afghanistan. Hivi sasa Marekani inafanya juhudi kubwa kuonyesha kwamba Daesh ni tishio kwa maslahi ya Washington nchini Afghanistan. Katika hali ambayo hadi sasa haijathibiti kwamba Daesh ni tishio kwa usalama wa Marekani ndani ya nchi hiyo." Iwapo Marekani inataka kutumia kisingizio cha kupambana na kundi la Daesh kwa madai kuwa ni tishio kwa maslahi yake ndani ya nchi hiyo, hivyo kuendelea kuwepo kijeshi nchini Afghanistan kutavunja moja kwa moja makubaliano iliyoyatia saini mjini Doha na kundi la Taleban na hivyo kulifanya kundi hilo kuanzisha tena vita na ukatili nchini humo.

Tags

Maoni