Jun 04, 2020 12:46 UTC
  • Barack Obama
    Barack Obama

Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama ametoa wito wa kufanyika marekebisho katika mfumo wa jeshi la polisi la nchi hiyo na kusisitiza kuwa, waandamanaji wanaopinga ubaguzi wa rangi wanapaswa kuwanyima utulivu wanaoshikilia madaraka.

Barack Obama amesema katika ujumbe wake wa video kwamba, maandamano ya sasa nchini Marekani dhidi ya ubaguzi hayawezi hata kufananishwa na yale ya muongo wa 1960 na amewataka mameya na magavana wa majimbo ya Marekani kufanya marekebisho katika vigezo vya utumiaji wa nguvu wa vyombo vya polisi.

Obama amesema kuwa, 

Ukatili na dhulma ambavyo ndiyo sababu ya maandamano ya sasa kote nchini vinahitaji kufanyiwa marekebisho.

Amesema maandamano ya sasa nchini Marekani ni matoko na harakati na ushiriki mkubwa wa idadi kubwa ya vijana kote nchini. 

Wakati huo huo Spika wa Bunge la Marekani Nancy Pelosi amejiunga na waandamanaji wanaopinga ubaguzi wa rangi na sera za ukatili za Rais Donald Trump wa nchi hiyo.

Nancy Pelosi

Pelosi alijiunga na waandamanaji wanaopinga mauaji yaliyofaywa na polisi dhidi ya raia mweusi, Georg Floyd, mbele ya jingo la Kongresi ya Marekani mjini Washington DC na kuwahamasisha akiwapigia makofi.

Spika wa Kongresi ya Marekani ambaye ni miongoni mwa wakosoaji wakali wa siasa za Trump, alikuwa tayari amesema kuwa, badala ya kufanya jitihada za kuwaunganisha Wamarekani, Donald Trump anachochea moto wa ghasia na maandamano ya ndani.

Machafuko hayo yamechochewa zaidi na matamshi ya kijuba, kibaguzi na ya jeuri ya rais wa nchi hiyo Donald Trump ambaye amewaita wanaolalamikia ukatili huo kuwa ni vibaka, wahuni na majambazi.

Wananchi wa Marekani wamekuwa wakiandamana kwa zaidi ya wiki moja sasa, tangu na polisi mweupe alipomuuawa kinyama George Floyd, Mmarekani mweusi, katika mji wa Minneapolis jimboni Minnesota.Karibu watu 20 wameuawa katika ghasia na maandamano hayo na wengine zaidi ya 10,000 wametiwa mbaroni katika majimbo mbalimbali ya Marekani kwa kushiriki maandamano hayo ya kupinga ubaguzi na dhulma.

Tags

Maoni