Jun 05, 2020 11:59 UTC
  • Nancy Pelosi
    Nancy Pelosi

Spika wa Kongresi ya Marekani ametahadharisha kwamba, mpango wa Israel wa kutaka kutwaa ardhi nyingine ya Palestina ya Ukingo wa Magharibi (West Bank) utadhoofisha sera za vyama viwili vikuu vya Marekani, Democratic na Republican, za kuiunga mkono Tel Aviv.

Nancy Pelosi ambaye alikuwa akihutubia mkutano wa Wayahudi na Demokrasia kupitia njia ya video, amesema kuwa, mpango huo wa Israel haukubaliki na unahatarisha mustakbali. 

Matamshi hayo ya Spika wa Bunge la Marekani ni sehemu ya upinzani mkali wa jamii ya kimataifa dhidi ya uamuzi wa utawala ghasibu wa Israel wa kutwaa ardhi ya Ukingo wa Magharibi. 

Kuhusu mpango habithi na wa kishetani wa Donald Trump uliopewa jina la Muamala wa Karne eti kwa ajili ya amani ya Mashariki ya Kati, Nancy Pelosi amesema kuwa, mpango huo haufanani hata kidogo naneno "amani".

Pelosi auponda Muamala wa Karne

Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel Benjamin Netanyahu ametangaza kwamba, kuanzia tarehe Mosi Julai atayaunganisha maeneo ya Palestina ya Ukingo wa Magharibi na ardhi zainazokaliwa kwa mabavu na utawala huo. Suala hilo limepingwa vikali na jamii ya kimataifa. 

Uamuzi huu ni sehemu ya vipengee vya mpangp wa kishetani wa Muamala wa Karne uliobuniwa na Rais Donald Trump wa Marekani na kuzinduliwa rasmi tareh 28 Januari mwaka huu.    

Tags

Maoni