Jul 01, 2020 11:28 UTC
  • Biden: Trump amesalimu amri mbele ya corona

Mgombea wa chama cha Democratic katika uchaguzi wa rais wa mwaka huu nchini Marekani amesema kuwa Rais wa nchi hiyo, Donald Trump amesalimu amri katika medani ya kupambana na maambukizi ya virusi vya corona na kupeperusha bendera nyeupe.

Akizungumza jana usiku katika jimbo la Delaware nchini Marekani, Joe Biden alimkumbusha Rais Trump matamshi yake kuhusu mapambano dhidi ya maambukizi ya corona pale alipojigamba kwamba ni rais wa kipindi cha vita na kueleza kuwa: Sasa umeingia mwezi Julai na inaonekana kuwa Trump amesalimu amri mkabala na corona na kuondoka katika uwanja wa vita. 

Mgombea huyo wa chama cha Democratic katika uchaguzi wa rais mwaka huu huko Marekani amemhutubua Trump akisema: Hatua alizochukua mpaka sasa hazijasaidia lolote na kwa msingi huo kabla ya kwenda kucheza mchezo wa golf anapasa kwanza awadhaminie wafanyakazi wa sekta ya afya suhula za kujikinga na maambukizi ya corona. 

Rais Donald Trump wa Marekani  

Takwimu rasmi zinaonyesha kuwa hadi sasa watu milioni 2 na 727,996 wameambukizwa virusi vya corona nchini Marekani. Watu 130,123 miongoni mwao wameaga dunia kwa ugonjwa wa Covid-19 nchini humo. 

Tags

Maoni