Jul 07, 2020 02:30 UTC
  • Associated Press: Wakuruba wa Trump wamepora mabilioni ya dola za corona

Kundi moja la ukaguzi nchini Marekani limefichua kwamba watu wa karibu na Rais Donald Trump wa nchi hiyo wamepora na kutafuna mabilioni ya dola zilizokuwa zimetengwa kama bajeti ya kuwasaidia waathirika wa virusi vya corona.

Shirika la habari la Associated Press limeripoti kuwa, kundi la usimamizi la Public Citizen limefichua kuwa, watu 40 wa karibu na Rais Donald Trump wa Marekani wamekuwa na nafasi kubwa katika kupora dola bilioni 10 zilizotengwa kama bajeti ya kuwasaidia watu waliopatwa na madhara kutokana na mgogoro wa virusi vya corona. 

Ripoti hiyo imeongeza kuwa, baadhi ya watu hao walikuwa wafanyakazi katika serikali ya Trump, wanachama katika timu yake ya kampeni za uchaguzi, wajumbe katika kamati ya kukusanya misaada ya kifedha na wanachama katika tume ya kukabidhi madaraka ya rais. 

Ripoti hiyo imesema baadhi ya mafisadi hao ni wachangishaji wakubwa wa bajeti ya kampeni za Donald Trump kwa ajili ya uchaguzi wa rais uliopangwa kufanyika Novemba mwaka huu.

Wakuruba wa Trump wamepota mabilioni ya dola

Ripoti ya kundi la Public Citizen imeongeza kuwa, miongoni mwa mafisadi hao ni Brian Ballard ambaye ni mwenyekiti wa kitengo cha fedha cha Kamati ya Taifa ya chama cha Republican ambaye amekusanya zaidi ya dola milioni moja kwa kamati ya misada ya kifedha ya timu ya kampeni za uchaguzi ya Donald Trump.

Mfisadi mwingine katika kashfa hiyo ni David Urban ambaye ni mshauri na mlinda siri mkubwa wa Donald Trump. 

Tags

Maoni