Jul 07, 2020 11:00 UTC
  • Baraza la Congress la Marekani lapasisha bajeti ya kulinda usalama wa Israel

Baraza la Wawakilishi la Marekani limepasisha bajeti ya kulinda usalama wa utawala wa Kizayuni wa Israel.

Gazeti la Kizayuni la Jerusalem Post limeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, wabunge wa Marekani wamepasisha bajeti ya mwaka 2021 ya zaidi ya dola bilioni tatu kwa ajili tu ya kulinda usalama Israel.

Kupasishwa bajeti  ya  bilioni 3.3 ya kulinda usalama wa utawala wa Kizayuni ni sehemu ya makubaliano yaliyofikiwa baina ya Marekani na Israel ya kuusaidia kijeshi utawala huo pandikizi na dhalimu.

Baraza la Congress la Marekani

 

Kamati ya Bajeti ya Baraza la Wawakilishi la Marekani imetangaza kuwa, kupasishwa bajeti hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi za Marekani katika makubaliano ya Camp David ya mwaka 1979. Kwa mujibu wa makubaliano hayo, Marekani ilitoa ahadi ya kutenga kiwango maalumu cha fedha cha kuusaidia utawala wa Kizayuni wa Israel pamoja na Misri.

Kamati hiyo imedai pia kuwa, muswada wa bajeti ya mwaka 2021 ya Marekani, umetenga pia dola milioni 225 kwa ajili ya Wapalestina, kama vile kuusaidia wakala wa UNRWA wa Umoja wa Mataifa unaoshughulikia masuala ya Palestina.

Hii ni katika hali ambayo mwaka 2018, Donald Trump alitangaza kukata misaada ya Marekani kwa taasisi hiyo inayowasaidia Wapalestina.

Tags

Maoni