Jul 14, 2020 02:33 UTC
  • UN yatahadharisha kuhusu athari mbaya za mauaji ya kigaidi ya Qassem Soleimani

Ripota maalumu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia mauaji ya kiholela na kinyume cha sheria ametahadharisha kuhusiana na athari mbaya za ugaidi unaofanywa na Marekani duniani hususan mauaji yaliyofanywa na nchi hiyo dhidi ya aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi al Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran, Luteni Jenerali Qassem Soleimani.

Agnès Callamard amewaambia waandishi habari kwamba, mauaji ya kigaidi yaliyofanywa na Marekani dhidi ya Qassem Soleimani yameonyesha ni kwa kiwango gani dunia inakaribia kwenye mgogoro mkubwa na wa maangamizi.

Callamard ameongeza kuwa, yumkini baadhi ya nchi zikatumia stratijia ya kuwaua maafisa wa kijeshi wa nchi nyingine kinyume cha sheria na kuhalalisha mauaji hayo kwa kudai kuwa walikuwa tishio lakini ukweli ni kwamba, suala hilo linaonesha mustakbali wenye maangamizi unaoikabili dunia. 

Ripota maalumu wa Umoja wa Mataifa amesisitiza udharura wa kukabiliana na sera hatari za kufanya vita kuwa jambo la kawaida na la dharura.

Awali Ripota Maalumu wa Umoja wa Mataifa alikuwa amesema Marekani imeiweka dunia katika hatari kubwa ambayo haijawahi kushuhudiwa tena kutokana na hatua ya jeshi lake kumuua Luteni Jenerali Qassem Soleimani, kamanda shahidi wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC).

Luteni Jenerali Qassem Soleimani na Abu Mahdi al-Mohandes waliuawa na drone za Marekani mapema mwaka huu.

Agnès Callamard alisema hayo jana Alkhamisi iliyopita wakati akikabidhi ripoti yake juu ya mauaji hayo ya kigaidi kwa Baraza la Haki za Binadamu la UN na kusisitiza kuwa, wakati umefika kwa jamii ya kimataifa kuvunja kimya chake juu ya mauaji ya kiholela yanayofanywa na Washington kwa kutumia ndege zisizo na rubani 'drone.' 

Januari 3 mwaka huu, jeshi la kigaidi la Marekani kwa amri ya rais wa nchi hiyo Donald Trump lilimuua kigaidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani na Abu Mahdi al-Mohandes, Naibu Mkuu wa Harakati ya Wananchi ya Hashdu al-Shaabi pamoja na watu waliokuwa wamendamana nao karibu wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baghdad akiwa mgeni rasmi wa serikali ya Iraq.

Tags

Maoni