Aug 03, 2020 11:29 UTC
  • Russia yaunga mkono haki ya Iran ya kustafidi na nishati ya nyuklia

Mwakilishi wa Russia katika taasisi za kimataifa zenye makao yao mjini Vienna Austria amesema kuwa Russia itaunga mkono haki ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ya kustafidi na nishati ya nyuklia.

Mikhail Ulyanov amemjibu Mark Dubowitz Mkuu wa Utendaji wa Taasisi ya Kutetea Demokrasia (FDD) yenye makao yake huko Washington na yenye mfungamano na utawala wa Kizayuni na kuandika katika ukurasa wake wa twitter kuwa: Iran inayo haki ya kustafidi na nishati ya nyuklia kwa mujibu wa mkataba wa NPT na suala hilo ni la kisheria. Mark Dubowitz ameandika katika ukurasa wake wa twitter kuwa, Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) kinyume na Iran imejizuia kuzalisha mada za radioactive nchini humo ambazo zinaweza kutumiwa kuundia bomu la nyuklia. 

Ujerumani, Uingereza na Ufaransa baada ya Marekani kujitoa kwa upande mmoja katika mapatano ya nyuklia ya JCPOA Mei 8 mwaka juzi 2018 ziliahidi kuwa zitaidhaminia Iran maslahi yake ya kiuchumi na hivyo kuyalinda mapatano hayo, lakini nchi hizo hadi sasa hazijachukua hatua yoyote ya maana kivitendo katika uwanja.  

Marekani baada ya kujitoa katika mapatano ya JCPOA 

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Mei 8 mwaka jana 2019  ilichukua hatua ya kupunguza uwajibikaji wake hatua kwa hatua kwa mujibu wa makubaliano ya JCPOA yaani mwaka mmoja baada Marekani kuvunja ahadi zake na pande za Ulaya kutochukua hatua yoyote ya kivitendo katika uwanja huo. 

 

Tags

Maoni