Aug 04, 2020 11:21 UTC
  • Trump: Kuingilia masuala ya magharibi mwa Asia ni kosa kubwa la kihistoria

Rais wa Marekani amekiri kuwa kitendo cha kuingilia masuala ya eneo la magharibi mwa Asia lilikuwa kosa kubwa katika historia ya nchi hiyo.

Donald Trump amesema katika mahojiano na tovuti ya habari ya Marekani ya Axios kuwa, lilikuwa kosa kubwa katika historia ya Marekani kitendo cha kuwatuma wanajeshi wa nchi hiyo huko Magharibi mwa Asia na kisha kuingilia masuala ya eneo hilo. 

Rais wa Marekani amedai pia kuwa, amefanya mambo mengi katika duru ya uongozi wake; kazi ambazo hazikufanywa katika zama za utawala wa Marais wa zamani wa Marekani. Katika mahojiano hayo Trump amedai kuwa Washington ndio iliyoliangamiza kundi la kigaidi la Daesh.  

Rais Trump amezungumzia pia suala la kupunguza wanajeshi wa Marekani walioko Afghanistan katika kipindi kifupi na kufikia elfu nane na kisha wanajeshi hao watapunguzwa tena hadi elfu nne. 

Amesema tukio hilo litajiri hivi karibuni hata hivyo hakutangaza tarehe rasmi ya kupunguzwa wanajeshi hao. 

Marekani na nchi waitifaki wake waliivamia Afghanistan mwaka 2001 kwa kisingizio cha kupambana na ugaidi na kuidhaminia usalama nchi hiyo hata hivyo kuanzia wakati huo hadi sasa hali ya mchafukoge, ukosefu wa amani, ugaidi na uzalishaji wa madawa ya kulevya vimeongezeka pakubwa huko Afghanistan. 

Uzalishaji wa madawa ya kulevya aina ya heroine nchini Afghanistan waongezeka pakubwa katika kalibu ya vikosi ajinabi

 

Tags

Maoni