Aug 09, 2020 03:26 UTC
  • IAEA yatakiwa kuwa na uwazi kuhusu mpango wa nyuklia wa siri wa Saudi Arabia

Kadhim Gharibabadi Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika taasisi za kimataifa mjini Vienna, Austria ametoa wito kwa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) uwe na uwazi kuhusu mpango wa siri wa nyuklia wa Saudi Arabia.

Gharibabadi amesema Saudi Arabia hivi sasa inastawisha na kutekeleza mradi wa nyuklia usio na uwazi na kuongeza kuwa: "Pamoja na kuwa Saudia ni mwanachama wa mkataba wa NPT wa kuzuia kuenezwa silaha za nyuklia lakini haijakubali miradi yake ya nyuklia ikaguliwe na Wakala wa Kimataifa wa Nyuklia."

Gharibabadi  ameongeza kuwa, Saudia imepuuza maombi ya IAEA ya kukaguliwa vituo vyake vya nyuklia pamoja na kuwa imetakiwa iwe na uwazi.

Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika taasisi za kimataifa mjini Vienna, amesema Saudia haina tanuri nyuklia la utafiti ili iwe na ulazima wa kuzalisha keki ya njano na kuongeza kuwa: "Kadhia hii pamoja na hatua za siri za Saudia na kukataa kwake kuwaruhusu wakaguzi wa IAEA pamoja na sera haribifu za nchi hiyo katika eneo ni mambo ambayo yanatia wasi wasi kuhusu mpango wa siri wa silaha za nyuklia wa Saudia.

Kituo cha nyuklia

Gharibabadi amesisitiza kuwa, IAEA na nchi za dunia zinapaswa kukabiliana ipasavyo na ukengeukaji wa mpango wa nyuklia wa amani na kuongeza kuwa, iwapo Saudia inataka kutumia nishati ya nyuklia kwa malengo ya amani lazima itekeleze majukumu yake mbele ya IAEA na iwe na uwazi kamili.

Tags

Maoni