Aug 10, 2020 08:07 UTC
  • Watu 21 wapigwa risasi mjini Washington, DC Marekani

Watu 21 wamepigwa risasi katika mji mkuu wa Marekani, Washington DC, ambapo hadi sasa mtu mmoja anaripotiwa kupoteza maisha.

Ufyatulianaji risasi huo ulijiri Jumapili asubuhi kwa saa za Washington katika mtaa ulio kusini mwa mji huo. 

Taarifa zinasema ufyatulianaji risasi ulijiri katika baa kufuatia mzozo wa kifamilia. Mkuu wa Polisi Washington DC Peter Newsham amesema watu kadhaa walifyatua risasi ambapo kijana aliyekuwa na umri wa miaka 17, Christopher Brown aliuawa. Aidha amesema afisa mmoja wa polisi alijeruhiwa vibaya katika tukio hilo na hali yake ni mahututi.

Katika miaka ya hivi karibuni, Marekani imeshuhudia ongezeko kubwa la vitendo vya uhalifu unahusisha ufyatulianaji risasi. 

Maelfu ya raia wa Marekani huuawa kila mwaka katika matukio ya mashambulizi ya silaha za moto katika maeneo tofauti ya nchi hiyo. Vitendo vya ukatili wa silaha za moto nchini Marekani vimegeuka kuwa moja ya matatizo makubwa na sugu katika jamii ya Marekani ambayo imezoea kuzinyooshea kidole cha lawama nchi nyingine za dunia kuhusiana na ukosefu wa amani.

Trump anaunga mkono umiliki wa bunduki Marekani

Makundi ya haki za raia yamekuwa yakitaka kuwepo sheria za kubana umiliki wa bunduki mikononi mwa raia.

Hata hivyo, Rais wa Marekani, Donald Trump anaunga mkono sheria inayoruhusu kuuzwa na kumiliki bunduki kiholela nchini humo.

Wamiliki wa mashirika makubwa ya kutengeneza silaha nchini Marekani wengi wao ni Wazayuni na wana ushawishi mkubwa katika Congress na Ikulu ya Marekani (White House), hivyo hawaruhusu kubanwa biashara ya silaha zinazozalishwa na mashirika hayo.

Tags

Maoni