Sep 11, 2020 14:22 UTC
  • Mahakama ya Marekani yataka kusailiwa maafisa wanne wa Saudi Arabia kwa kuhusika na mashambulizi ya Septemba 11

Baada ya mashambulizi ya Septemba 11 mwaka 2001 Marekani ilijinadi kuwa kinara wa mapambano dhidi ya ugaidi duniani na ikachukua hatua ya kuzivamia nchi za Iraq na Afghanistan.

Hata hivyo Washington imekuwa na sera zinazokinzana katika uwanja huo. Hii ni kutokana na ukweli kwamba, serikali ya sasa ya nchi hiyo inayoongozwa na Donald Trump inafanya jitihada kubwa za kuficha nafasi ya Saudi Arabia katika mashambulizi ya kigaidi ya Septemba 11 katika miji ya New York na Washington huku vyombo vya mahakama vya Marekani vikiendelea kutoa wito wa kuwekwa wazi nafasi ya maafisa wa ngazi za juu wa Saudia katika tukio hilo. 

Katika uwanja huu jaji wa Mahakama ya Federali ya Marekani ametoa wito wa kusailiwa maafisa wanne wa ngazi za juu wa Saudi Arabia kuhusu uwezekano kwamba walikuwa na habari ya mpango wa mashambulizi ya Septemba 11. Miongoni mwa maafisa hao ni Bandar bin Sultan aliyekuwa balozi wa Saudia mjini Washington. Wakati huo huo Giil Santiborne ambaye ni afisa wa ngazi za juu wa shirika la upelelezi la FBI hivi karibuni aliwasilisha mahakamani waraka unaothibitisha kuwa, mwanadiplomasia wa Saudia, Mussaed Ahmed al-Jarrah, ni "mtu wa tatu" aliyehusika katika mashambulizi ya Septemba 11 mwaka 2001 na kwamba alitoa msaada kwa magaidi wa kundi la al Qaida. Baada ya hapo msemaji wa familia za wahanga wa mashambulizi ya Septemba 11 alisema kuwa, suala hilo linaonesha kuwa, serikali ya Marekani inanyamazia kimya nafasi ya Saudi Arabia katika mashambulizi hayo. ambaye ni afisa wa ngazi za juu wa shirika la upelelezi la FBI siku chache zilizopita aliwasilisha waraka mahakamani waraka unaothibitisha kuwa, mwanadiplomasia wa Saudia, Musaid Ahmad al Jarrah, ni "mtu wa tatu" aliyehusika katika mashambulizi ya Septemba 11 mwaka 2001 na kwamba alitoa msaada kwa magaidi wa kundi la al Qaida. Baada ya hapo msemaji wa familia za wahanga wa mashambulizi ya Septemba 11, Brett Eagleson alisema kuwa, suala hilo linaonesha kuwa, serikali ya Marekani inanyamazia kimya nafasi ya Saudi Arabia katika mashambulizi hayo.

Bandar bin Sultan

Katika miaka kadhaa iliyopita tangu baada ya mashambulizi ya Septemba 11, Saudia ambayo ndiye mtuhumiwa mkuu wa mashambulizi hayo, imetumia kiasi kikubwa cha fedha na vyombo vya habari kwa ajili ya kujinasua kwenye tuhuma hiyo. Ripoti iliyotolewa na Kongresi ya Marekani mwezi Julai mwaka 2016 kuhusiana na tukio la Septemba 11 ilieleza waziwazi kwamba magaidi 15 kati ya 19 walioteka nyara ndege za abiria na kuzitumia katika mashambulizi ya Septemba 11, walikuwa raia wa Saudi Arabia. 

Suala hilo liliifanya Kongresi ya Marekani ipasishe sheria ya JASTA inayoziruhusu familia za wahanga wa mashambulizi hayo kufungua mashtaka dhidi ya serikali na maafisa wa Saudi Arabia kwa sababu ya kuwasaidia magaidi waliohusika na tukio la Septemba 11 mwaka 2001. Hata hivyo serikali ya Barack Obama na hii ya sasa na Doland Trump zimezuia utekelezaji wa sheria hiyo ya JASTA kwa kisingizio kwamba, itakuwa na taathira mbaya kwa uhusiano wa Washington na Riyadh. Msimamo huu unaonesha waziwazi sera za kinafiki na zinazogongana za Marekani katika suala la kupambana na ugaidi. Serikali ya Trump imefumbia macho kabisa nafasi ya Saudi Arabia ya kuyalea kiitikadi makundi ya kigaidi ya al Qaeda na Daesh na kuyafadhili kwa fedha na silaha.

Trump na Bin Salman

Nukta nyingine inayopaswa kuzungumziwa kuhusiana na mashambulizi ya Septemba 11 mwaka 2001 ni sababu za tukio hilo na jinsi Marekani ilivyolitumia kama fursa na kisingizio cha kuhujumu na kuzivamia nchi mbalimbali hususan za magharibi mwa Asia. Kimsingi tunaweza kusema kuwa, mashambulizi ya Septemba 11 yalikuwa jibu kwa hatua za Marekani za kuzidisha majeshi yake katika Ulimwengu wa Kiislamu hususan baada ya vita vya kwanza vya Ghuba ya Uajemi ambapo nchi za Magharibi zilituma malaki ya wanajeshi  wao katika eneo hilo. Kwa maneno mengine ni kuwa, tukio la Septemba 11 mwaka 2001 lina mizizi katika sera za Marekani za kuingilia masuala ya ndani ya nchi nyingine baada ya vita vya kwanza vya Ghuba ya Uajemi. Uwepo wa majeshi ya Marekani na waitifaki wake katika eneo hilo ulikuwa mkubwa sana kwa kadiri kwamba, suala hilo lilipelekea kujitokeza mrengo wenye nguvu kubwa wa kisiasa na kifikra uliohimiza udharura wa kukabiliana na hali hiyo. Kundi la al Qaida lilitumia hali hiyo na baadaye kulitokea mashambulizi ya Septemba 11 kwa msaada wa kifedha na kilojestiki wa maafisa wa ngazi za juu wa Saudia akiwemo balozi wa zamani wa nchi hiyo mjini Washington, Bandar bin Sultan. 
Pamoja na hayo, badala ya kukabiliana na kuusaili utawala wa Aal Saud, Washington daima imekuwa ikifanya juhudi za kuficha suala hilo na wakati huo huo kutumia tukio la Septemba 11 kama mwavuli wa kutekeleza mipango yake na kuzihujumu nchi nyingine kwa kisingizio cha kupambana na ugaidi. Matokeo ya mashamblizi na hujuma hizo za Marekani ni mauaji ya maelfu ya raia wasio na hatia katika nchi kama Iraq, Afghanistan, Somalia, Syria na kadhalika na vilevile kuundika kwa makundi mengine ya kigaidi kama Daesh. 

Maelfu ya Waafghani wameuawa katika mashambulizi ya Marekani

Nukta nyingine ni kwamba vita vya Marekani nje ya nchi hiyo baada ya Septemba 11 mwaka 2001 vimesababisha hasara kubwa ya fedha. Katika uwanja huu Rais Donald Trump anadai kuwa, vita na hujuma hizo zimeigharimu Marekani zaidi ya dola trilioni 7. Gharama hizi kubwa zimeisababishia Marekani nakisi ya bajeti na madeni makubwa ya taifa na matokeo yake ni kusahauliwa jukumu la Serikali ya Federali la kuboresha miundombinu ya nchi na kupungua bajeti ya masuala ya afya, elimu na jamii. 
Nukta ya mwisho tunayoashiria ni kwamba vita vya Marekani baada ya Septemba 11 badala ya kuzidisha amani na usalama wa dunia, vimekuwa sababu ya kuongezeka hali ya ukosefu wa amani, ugaidi na machafuko katika maeneo tofauti ya dunia. 

Tags