Sep 17, 2020 13:07 UTC
  • Trump ndiye kiongozi mbovu zaidi duniani katika suala la kukabiliana na virusi vya corona

Matokeo ya uchunguzi mpya wa maoni uliofanywa nchini Marekani yanaonyesha kuwa rais wa nchi hiyo Donald Trump ndiye kiongozi mbovu zaidi duniani katika kukabiliana na janga la ugonjwa wa Covid-19 unaosababishwa na virusi vya corona.

Televisheni ya CNN imeripoti kuwa uchunguzi mpya wa maoni uliofanywa na taasisi ya utafiti ya PEW unaonyesha kuwa utendaji wa rais Donald Trump wa Marekani katika kukabiliana na janga la corona ni dhaifu zaidi kuliko wa marais Vladimir Putin wa Russia na Xi Jinping wa China.

Uchunguzi huo wa taasisi ya PEW waliofanyiwa watu wa nchi 13 duniani unaonyesha pia kuwa haiba ya Marekani mbele ya raia wa nchi hizo imeshuka.

Kwa mujibu wa uchunguzi huo, kwa wastani, ni asilimia 15 tu ya watu wa nchi hizo 13 wana mtazamo kuwa serikali ya Marekani imechukua hatua nzuri na za maana katika kukabiliana na janga la corona.

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani

Matokeo ya uchunguzi huo wa maoni uliofanywa na taasisi ya PEW yanaonyesha kuwa Kansela Angela Merkel wa Ujerumani ni kiongozi ambaye amekuwa na utendaji wa mafanikio katika kukabiliana na janga la corona akilinganishwa na viongozi wengine duniani.

Huku zikiwa zimesalia chini ya siku 50 kabla ya kufanyika uchaguzi wa urais wa Marekani, Trump anahaha kutafuta uungaji mkono wa wapigakura wa nchi hiyo.

Mshindani wake mkuu Joe Biden, anayewania urais kwa tiketi ya chama cha Democrat amesema, hadi ifikapo mwanzoni mwa mwaka ujao wa 2021, zaidi ya Wamarekani laki mbili na nusu watakuwa wameshafariki dunia kutokana na ugonjwa wa Covid-19 na akasisitiza kuwa kushindwa Trump kuudhibiti ugonjwa huo kunamfanya apoteze sifa za kustahiki kuwa rais wa nchi.../

Tags

Maoni