Sep 18, 2020 10:38 UTC
  • Trump aendelea kubwabwaja, asema atafanya mapatano na Iran katika kipindi cha wiki moja

Rais Donald Trump wa Marekani jana Alkhamisi aliendelea kuona ndoto za mchana za kutaka kufikia mapatano na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kudai kwamba, iwapo atachaguliwa tena kuiongoza Marekani atafikia mapatano na Iran katika kipindi cha wiki moja.

Trump aliendelea kutoa matamshi ya dhihaka akidai kuwa Iran inasumuliwa na tatizo la kupungua uzalishaji ghafi wa ndani wa asilimia 27 na kusema: Kuna uwezekano mkubwa kwamba Tehran itafanya muamala na Washington.

Katika miezi ya karibuni Rais wa Marekani na maafisa wengine wa ngazi za juu wa nchi hiyo akiwemo Waziri wa Mambo ya Nje, Mike Pompeo, wamekuwa wakiomba kufanya mazungumzo na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa njia moja au nyingine.

Trump na maafisa wenzake wa Marekani wametoa ombi hilo la kufanya mazungumzo na Iran ilhali mwaka 2018 waliiondoa kinyume cha sheria nchi hiyo katika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA yaliyoidhinishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Hatua hiyo imelaaniwa ndani ya Marekani na katika medani ya kimataifa.

Siku chache zilizopita pia Rais wa Marekani alijigamba tena akidai kuwa iwapo Iran itachukua hatua yoyote ya kulipiza kisasi cha muaji ya kigaidi yaliyofanywa na jeshi la nchi hiyo dhidi ya Luteni Jenerali Qassem Soleimani, aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran, na kushambulia maeneo au maslahi ya Marekani, jibu la Washington litakuwa mara elfu moja zaidi. 

Donald Trump

Luteni Jenerali Qassem Soleimani na wenzake kadhaa waliuawa kigaidi Ijumaa ya tarehe 3 Januari katika shambulizi la Marekani karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baghdad. Kamanda Soleimani alikuwa safarini nchini Iraq kwa mwaliko rasmi wa Waziri Mkuu wa nchi hiyo.  

Ripota Maalumu wa Umoja wa Mataifa, Agnès Callamard, amekitaja kitendo hicho kuwa ni hujuma ya kigaidi.

 Kamanda Soleimani alikuwa kinara wa mapambano dhidi ya kundi la kigaidi la Daesh katika eneo la magharibi mwa Asia.

Maoni