Sep 20, 2020 02:40 UTC
  • Putin: Kujiondoa Marekani katika mkataba wa makombora kumeilazimisha Moscow kuunda makombora ya hypersonic

Rais Vladimir Putin wa Russia amesema kuwa hatua ya Marekani ya kujiondoa katika mkataba wa makombora hapo mwaka 2002 iliilazimisha Moscow kuanza mchakato wa kustawisha silaha zenye kasi kubwa kuliko sauti, (hypersonic missile).

Vladimir Putin amesema kuwa, baada ya uamuzi wa Marekani wa mwaka 2002 wa kuchana mkataba wa silaha za balestiki, Moscow haikuwa na njia nyingine ghairi ya kustawaisha zaidi mfumo wa silaha zenye kasi kubwa kuliko ya sauti.

Rais wa Russia amesema kuwa, hii leo na kwa mara ya kwanza katika historia ya sasa ya Russia nchi hii imeweza kuwa na silaha za kisasa kabisa ambazo ni bora zaidi katika upande wa nguvu, uwezo, kasi, na zaidi ya yote, umakini kuliko silaha zote za hapo kabla. 

Kombora la Avangard

Mwaka 2018 Russia ilizindua mfumo wa makombora yenye kasi kubwa kuzidi ya sauti wa Kinzhal na makombora yanayovuka mabara ya The Avangard; mwaka mmoja kabla ya wakati uliokuwa umepangwa kuzinduliwa. Silaha hizo zilitengenezwa kujibu hatua ya Marekani ya kutengeneza ngao ya kujikinga na makombora.    

Tags

Maoni