Sep 21, 2020 13:37 UTC
  • Mazoezi ya kijeshi ya Kavkaz-2020
    Mazoezi ya kijeshi ya Kavkaz-2020

Mazoezi ya pamoja ya kijeshi yaliyopewa jina la Kavkaz-2020 yamenza leo yakishirikisha wanajeshi elfu 13 kutoka nchi za Iran, China, Pakistan, Belarus, Myanmar na mwenyeji Russia katika eneo la kusini mwa nchi hiyo.

Wizara ya Ulinzi ya Rusia imetangaza kuwa, mazoezi hayo ya pamoja yanafanyika kwa shabaha ya kuimarisha hali ya kuaminiana na ushirikino kati ya nchi za kusini mwa Russia na kandokano ya Bahari ya Caspi na Bahari Nyeusi na vilevile kudhamini usalama wa maeneo hayo. 

Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Ulinzi ya Russia imesema kuwa, katika maneva hayo kunafanyika mazoezi ya jinsi ya kutumia vikosi vya jeshi vya muungano wa nchi kadhaa kwa ajili ya kudhamini usalama kusini magharibi mwa Russia na kwamba zana za kisasa kabisa za kivita na za kiulinzi, mifumo ya kujikinga na makombora, makumbora mapya, ndege za kivita, helikopta na kadhalika zinatumiwa katika mazoezi hayo.

Kavkaz-2020

Taarifa hiyo imeongeza kuwa, meli za kivita za Iran na Russia zitashiriki katika mazoezi ya baharini kwenye Bahari ya Caspi na Bahari Nyeusi. 

Mazoezi ya kijeshi ya Kavkaz-2020 yanafanyika katika awamu mbili kuanzia leo hadi tarehe 26 Septemba. 

Taarifa ya Wizara ya Ulinzi ya Russia imesema kuwa mazoezi hayo yanajikiza zaidi katika jinsi ya kukabiliana na makombora ya cruise na ndege zisizo na rubani. 

Tags

Maoni