Sep 21, 2020 13:40 UTC
  • Wabunge wa Ufaransa nao wapinga mapatano ya Imarati, Bahrain na Israel

Wabunge 61 wa Bunge la Ufaransa wamekosoa mapatano ya kuanzishwa uhusiano baina ya Imaratina Bahrain na utawala haramu wa Israel.

Wabunge hao wa Ufaransa wamesema kuwa, makubaliano ya nchi za Imarati na Bahrain ya kuanzisha uhusiano na utawala wa Israel yatatatiza juhudi za kutatua kadhia ya Palestina na kuondoa kabisa uwezekano wa kufikiwa mapatano na amani ya kudumu eneo la magharibi mwa Asia.

Wabunge 61 wa Ufaransa pia wamesema kuwa, makubaiayo yaliyotiwa saini White House kama yalivyotangazwa kwa shangwe na vifijo na Rais Donald Trump wa Marekni hayawezi kuitwa mkataba wa amani. 

Tarehe 15 mwezi huu wa Septemba mawaziri wa mambo ya nje wa nchi za Imarati na Bahrain walisaini mapatano ya kuanzisha uhusiano na utawala wa Kizayuni wa Israel na Waziri Mkuu wa utawala huo, Benjamin Netanyahu katika ikulu ya rais wa Marekani, White House mjini Washington.  Hatua hiyo ya Imarati na Bahrain imekosolewa na kupingwa vikali katika ulimwengu wa Kiislamu. 

Waislamu wanapinga mapatano ya aina yoyote ya utawala haramu wa Israel

Mahmoud al-Zahar ambaye ni mjumbe wa Idara ya Siasa ya Hamas amesema kuwa, hatua ya Imarati na Bahrain ya kuanzisha uhusiano na utawala wa Kizayuni wa Israel ni kulisaliti taifa la Palestina na kujiunga na kambi ya utawala ghasibu wa Israel kwa ajili ya kuangamiza kabisa mapambano ya kupigania uhuru ya Palestina. 

Al Zahar amesema kuwa, Imarati na Bahrain zimetenda jinai na uhalifu wa kisiasa, kimaadili na kihistoria dhidi ya watu wa Palestina wanaoendelea kusumbuliwa na mauaji na ukatili wa  Wazayuni katika ardhi yao tukufu.

Tags

Maoni