Sep 24, 2020 02:42 UTC
  • Venezuela yaunda kikosi maalumu cha makomando kukabiliana na chokochoko za Marekani

Rais Nicolas Maduro wa Venezuela ameukosoa vikali ujambazi na umafia unaofanywa na serikali ya Marekani dhidi ya nchi yake na ametangaza habari ya kuundwa kikosi maalumu cha makomando cha kupambana na vitendo vya kiharibifu vya Marekani.

Hayo yametangazwa na televisheni ya al Mayadeen ambayo imemnukuu Rais Maduro akitoa taarifa ya kikosi hicho maalumu cha kukabiliana na chokochoko na vita vinavyoweza kuanzishwa na Marekani nchini humo akisema kuwa, kikosi hicho maalumu kina uwezo wa kubadilisha maeneo yake masaa yote 24 kwa siku katika kila kona ya Venezuela.

Rais wa Venezuela vile vile amesema, hatua ya pili ya vikwazo vya Marekani dhidi ya viongozi wa nchi hiyo ni umafia wa kiserikali na kuongeza kuwa, kuwawekea vikwazo viongozi wa Venezuela ni kutafuta nafasi zaidi za kuwakandamiza wananchi wa nchi hiyo na hilo kusema kweli halifanywi ila na magenge ya kijambazi na kimafia tu.

Wanajeshi wa Venezuela wakiwa tayari kukabiliana na Marekani

 

Kabla ya hapo pia Rais Maduto aliwah kulituhumu shirika la kijasusi la Marekani CIA kuwa linafanya vitendo vya kijambazi, kimafia na kigaidi nchini mwake.

Juzi Jumanne, Wizara ya Hazina ya Marekani iliendeleza siasa za kiuadui na kidhulma za nchi hiyo kwa kutangaza kuwawekea vikwazo viongozi wengine watano wa Venezuela.

Katika miezi ya hivi karibuni, Marekani imetangaza vikwazo vya kiuchumi na kuchochea na kusaidia uharibifu wa miundombinu na wa kisiasa ndani ya Venezuela dhidi ya serikali iliyochaguliwa kidemokrasia kwa sababu tu serikali hiyo haitaki kuburuzwa na dola la kibeberu la Marekani na inapigania ukombozi wa wananchi wa nchi hiyo ya Amerika ya Latini.

Tags

Maoni