Sep 24, 2020 02:43 UTC
  • Ujerumani yamshutumu vikali Trump kwa kutoa amri ya kuuliwa Luteni Soleimani

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani amemshutumu na kumlaumu vikali rais wa Marekani, Donald Trump kwa kutoa amri ya kuuliwa Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Walinzi wa Mapiduzi ya Kiislamu SEPAH.

Haiko Maas amesema kuhusu jinai ya wanajeshi wa Marekani ya kumuua kigaidi na kidhulma Kamanda Qassem Soleimani kwamba, hatua hiyo ilikuwa ya hatari sana na ingeliweza kuzusha vita vikubwa katika eneo la Asia Magharibi.

Waziri huyo wa Mambo ya Nje wa Ujerumani vile vile amesema kuwa, Trump anatumia migogoro ya ndani ya Marekani kama nyezo za kuvutia wapiga kura na lengo lake hasa ni kushinda kwa njia yoyote ile katika uchaguzi ujao huko Marekani.

Tarehe 3 Januri mwaka huu wa 2020, Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH aliuliwa shahidi kidhulma na wanajeshi wa Marekani akiwa uraiani na tena akiwa mgeni rasmi wa serikali ya Iraq.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Haiko Maas

 

Wizara ya Ulinzi wa Marekani Pentagon ilisema, ilifanya mauaji hayo kwa amri ya moja kwa moja ya rais wa nchi hiyo, Donald Trump.

Nchi nyingi duniani, mashirika na makundi mbalimbali yamelaani vikali jinai hiyo ya Marekani iliyofanywa kiwoga, kwa kuvuzia na tena uraiani, si katika medani ya vita.

Iran inaendelea kusisitiza kuwa, kisasi cha jinai hiyo ya Marekani bado hakijatolewa na kwamba hatua ya Tehran kwa kuipiga kwa makombora kambi ya wanajeshi magaidi wa Marekani ya 'Ain al Assad huko Iraq ilikuwa ni sehemu ndogo tu ya majibu yake kwa magaidi hao. 

Tags

Maoni