Sep 25, 2020 11:14 UTC
  • Rais Maduro: Marekani inashirikiana na magenge ya madawa ya kulevya ya Colombia dhidi ya Venezuela

Rais Nicolas Maduro wa Venezuela amesema kuwa, Idara ya Kupambana na Madawa ya Kulevya ya Marekani inashirikiana na walanguzi wa madawa ya kulevya wa nchini Colombia kwa ajili ya kutoa pigo dhidi ya serikali ya Caracas.

Rais Maduro amesisitiza kuwa, Idara ya Kupambana na Madawa ya Kulevya ya Marekani imekuwa ikishirikiana na magenge ya Colombia yanayojihusisha na magendo ya madawa ya kulevya ili kuzusha vurugu na machafuko nchini Venezuela.

Rais wa Venezuela amelaani vikali hatua hizo za serikali ya Marekani na kueleza kwamba, zitashindwa vkama mipango mingine ya Washington ya kuisambaratisha serikali ya Caracas ilivyoshindwa.

Karibuni hivi pia, Rais Maduro alisema kuwa, Rais Donald Trump wa Marekani ametoa amari ya kutekelezwaoperesheni za siri za kigaidi dhidi ya Venezuela.

Rais Nicolas Maduro wa Venezuela

 

Rais Nicolas Maduro wa Venezuela amekosoa vikali ujambazi na umafia unaofanywa na serikali ya Marekani dhidi ya nchi yake na tyari ametangaza habari ya kuundwa kikosi maalumu cha makomando cha kupambana na vitendo vya kiharibifu vya Marekani.

Katika miezi ya hivi karibuni, Marekani imetangaza vikwazo vya kiuchumi na kuchochea sambamba na kusaidia uharibifu wa miundombinu na wa kisiasa ndani ya Venezuela dhidi ya serikali iliyochaguliwa kidemokrasia kwa sababu tu serikali hiyo haitaki kuburuzwa na dola la kibeberu la Marekani na inapigania ukombozi wa wananchi wa nchi hiyo ya Amerika ya Latini.

Hadi sasa njama zote za Marekani dhidi ya Venezuela zimefeli na kugonga mwamba kutokana na uungaji mkono wa wananchi na jeshi la nchi hiyo kwa Rais Maduro

Tags

Maoni