Sep 26, 2020 07:52 UTC
  • Siri ya Netanyahu na mkewe kubeba nguo chafu Marekani ili zikafuliwe bure hotelini yafichuka

Gazeti la Washington Post limefichua kuwa, Waziri Mkuu wa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel Benjamin Netanyahu amekuwa na mtindo wa kubeba nguo chafu anapokuwa katika ziara rasmi nchini Marekani ili zikafuliwe kwa gharama za serikali ya nchi hiyo badala ya yeye mwenyewe kulipia gharama za ufuaji.

Gazeti hilo limewanukuu maafisa wa serikali ya Marekani wakieleza kwamba, kila anapoelekea Washington kwa safari rasmi za kidiplomasia, Netanyahu na mkewe Sara huwa wanabeba masanduku yaliyojaa nguo chafu ili wakafuliwe bila malipo katika hoteli wanayofikia.

Kwa mujibu wa maafisa hao wa serikali ya Washington, kwa miaka kadhaa sasa, Netanyahu amekuwa maarufu kwa wafanyakazi wa nyumba za wageni wa rais wa Marekani kutokana na tabia yake ya kubeba mizigo maalumu anapokuwa safarini mjini Washington, ambayo ni ya mikoba na masanduku yaliyojaa nguo chafu.

Kwa mujibu wa ripoti ya Washington Post, nguo hizo huwa zinafuliwa bila malipo na wafanyakazi wa nyumba za wageni wa rais wa Marekani.

Netanyahu na mkewe Sara

Afisa mmoja wa serikali ya Marekani ambaye hakutaka jina lake litajwe, ameliambia gazeti hilo: "Netanyahu ni kiongozi pekee anayetuletea mabegi ya nguo chafu kutaka afuliwe." Afisa huyo ameongeza kuwa: "Baada ya safari kadhaa ilibainika kuwa anafanya hivyo makusudi."

Tovuti ya habari ya gazeti la Israel Times imenukuu ripoti zake kadhaa ilizowahi kutoa huko nyuma kuhusu tabia hiyo ya ajabu ya waziri mkuu wa utawala wa Kizayuni na kuandika kuwa: Ripoti za Washington Post zinatilia nguvu uvumi ambao umekuwepo kwa muda wa miaka 10 kuhusu hulka ya Netanyahu na mkewe ya kupenda kufulisha nguo zao chafu bila malipo.../ 

Tags

Maoni