Sep 29, 2020 01:30 UTC
  • Ufichuzi; Trump amekwepa kulipa kodi ya mapato kwa miaka 10

Imebainika kuwa, Rais wa Marekani Donald Trump amekuwa akikwepa kulipa kodi ya mapato katika kipindi cha miaka 10 kati ya 15 iliyopita.

Gazeti la The New York Times limefichua kuwa, Trump alilipa kodi ya mapato ya dola 750 tu mwaka 2016 alipochaguliwa kushika hatamu za uongozi, na kwamba amekuwa akikwepa kulipa kodi kwa muda wa miaka 10 tokea mwaka 2000.

Ufichuzi huo wa New York Times umewaghadhabisha wananchi wa Marekani ambao wanakabiliwa na hali ngumu ya maisha, mdororo wa uchumi na mfumko wa bei za bidhaa.

Haya yanajiri wakati huu ambapo utawala wa Trump unaendelea kukosolewa kwa namna ulivyoshindwa kulishughulikia janga la COVID-19. Kadhalika ufichuzi huu umekuja masaa machache kabla ya kufanyika mdahalo wa urais baina yake na Joe Biden, mgombea urais wa Marekani kwa tiketi ya chama cha Democrat leo Jumanne.

Maandamano ya Wamarekani ya kutaka Trump afichue vyanzo vya utajiri wake na rekodi ya kulipa ushuru

 

Trump ambaye ni mchezaji kamari mkubwa amekuwa akikwepa mashinikizo ya kumtaka atangaze hadharani vyanzo vya utajiri wake.

Hivi karibuni, Biden alisema Donald Trump ni rais fisadi zaidi katika historia ya sasa ya nchi hiyo kwa namna anavyotumia vibaya mamlaka yake kwa ajili ya kuwanufaisha watu wake wa karibu.

Tags

Maoni